Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CAR : UN yalaani vikali mashambulizi ya waasi Damara na Bangassou 

Walinda amani wa MINUSCA wakiongeza doria na kulinda raia kwenye eneo la Bangassou nchini CAR kufuatia mashambulizi ya Januari 3.
MINUSCA
Walinda amani wa MINUSCA wakiongeza doria na kulinda raia kwenye eneo la Bangassou nchini CAR kufuatia mashambulizi ya Januari 3.

CAR : UN yalaani vikali mashambulizi ya waasi Damara na Bangassou 

Amani na Usalama

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR ujulikanao kama MINUSCA leo Jumapili umelaani vikali mashambulizi yaliyofanywa na makundi yenye silaha katika miji ya Ombella-M’poko jimboni Damara Jumamosi na Mbomou Bangassou leo Jumapili.


Katika taarifa yake mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu na mkuu wa MINUSCA Mankeur Ndiaye amesema “Hakuna shaka kwamba mashambulizi haya yamefanyika katika dhamira ya kuvuruga uchaguzi kabla, wakati na baada ya upigaji kura.”
Karibu watu milioni 2 nchini CAR walipiga kura Desemba 27 mwaka jana kuchagua Rais na wabunge licha ya majaribio kadhaa ya makundi ya waasi kutaka kuzuia kufanyika kwa uchaguzi huo.

Matokeo ya awali ya duru ya kwanza ya uchaguzi yanatarajiwa kutolewa kesho Januari 4. 
Bwana Ndiaye amesisitiza kwamba “Katika mukhtada wa azimio 2552 MINUSCA inawajibika kuhakikisha usalama wakati wa uchaguzi. Ninasisitiza dhamira yay a MINUSCA katika kutimiza ahadi hiyo.”


Mashambulizi Damara na Bangassou

Kwa mujibu wa mpango huo wa Umoja wa Mataifa mashambulizi yaliyofanyika Damara yametokea Jumamosi asubuhi baada ya askari waliokuwa wafuasi wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Francois Bozize kushambulia mji huo.


Jeshi la serikali FACA lilijibu mashambulizi hayo na kufanikiwa kuwafurusha washambuliaji, huku walinda amani wa MINUSCA wakiongeza doria mjini humo na maeneo ya jirani na maiti wanane wa waasi hao walipatikana.


Nako mjini Bangassou washambuliaji walianza mashambulizi dhidi ya kituo cha jeshi la FACA karibu saa 11:30 alfajiri leo Jumapili saa za CAR wakiwa na silaha nzitonzito.
“Walinda amani wa MINUSCA haraka walichukua hatua kuwalinda raia , kulinda malaka ya eneo hilo na kuendelea na kufanya doroa ya kina. Pia MINUSCA inahakikisha ulinzi kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani na imewasafirisha wanajeshi wawili wa FACA waliojeruhiwa kwenda kutibiwa Bria.” Imesema taarifa hiyo ya MINUSCA.


Kwa mujibu wa MINUSCA mashambulizi yalikoma karibu saa nne asubuhi saa za CAR lakini hali bado ni tete mjini humo ambako maiti zingine 5 za waasi wenye silaha ziliokotwa.


Mashambulizi haya ya karibuni kabisa yamefanyika wakati kukiripotiwa machafuko Magharibi mwa nchi hiyo ambayo yamesababisha safari za Ndege za rai ana misaada ya kibinadamu kwa maelfu ya walio na mahitaji kusitishwa.

Makundi yote yenye silaha yatawajibishwa kwa uasi wao


“Mpango wa MINUSCA unawashutumu UPC, MPC, 3R, FPRC, anti-Balaka na Rais wa zamani Francois Bozize kuhusika na mashambulizi hayo na athari mbaya za mashambulizi hayo kwa raia”. Imeendelea kusema taarifa ya MINUSCA na kuahidi kwamba mpango huo umejizatiti kuwalinda rai ana mamlaka kwa kuzingatia wajibu wake.


Na mwisho mpango huo umekumbusha tamko la Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa lililotolewa Desemba 19 mwaka jana la kulaani kuendelea kwa machafuko nchini CAR na kutoa wito kwa pande zote kusitisha uhasama mara moja, kufanya kila liwezekanalo kuwalinda raia na kutekeleza mkataba wa amani (PPA) ambao pande zote ziliutia saini.


“Mak yenye silaha yatawajibishwa kwa matendo yao kwa kufiata vikwazo zilivyowekwa na mkataba wa APPR undi yote“imemalizia taarifa hiyo ya MINUSCA.