Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto milioni 140 watazaliwa mwaka huu wa 2021. Wastani wa kuishi, miaka 84: Makadirio ya UNICEF  

Picha ya mwaka 2020 ikimwonesha mtoto wa kwanza katika mwaka huo aliyezaliwa katika Kituo cha afya cha Segou, Mali.
© UNICEF/Seyba Keïta
Picha ya mwaka 2020 ikimwonesha mtoto wa kwanza katika mwaka huo aliyezaliwa katika Kituo cha afya cha Segou, Mali.

Watoto milioni 140 watazaliwa mwaka huu wa 2021. Wastani wa kuishi, miaka 84: Makadirio ya UNICEF  

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limekadiria kuwa hadi siku hii ya kwanza yam waka itakapoisha, kuanzia Fiji, ambako mwaka mpya uliingia mapema hadi kule Marekani ambako wao waliuona mwaka kwa kuchelewa, kutakuwa na watoto 371,5004 watakaozaliwa kote ulimwenguni.  

Kwa mujibu wa UNICEF, inatarajiwa kwamba zaidi ya nusu ya "watoto wa Mwaka Mpya" watazaliwa katika nchi kumi zifuatazo: India (takriban 59,995), Uchina (35,615), Nigeria (21,439), Pakistan (1 4,164), Indonesia (12,336), Ethiopia (10,2006), Merika (10,312), Misri (9455), Bangladesh (9,236), na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC (8,640). 

Kupitia uchambuzi wa sensa ya kitaifa na data ya usajili, na pia ripoti ya Umoja wa Mataifa "Mtazamo wa Idadi ya Watu", UNICEF inakadiria kuwa jumla ya takriban watoto milioni 140 watazaliwa ulimwenguni mnamo 2021, wakiwa na wastani wa umri wa kuishi wa miaka 84. 

Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Fowler anasema, "watoto waliozaliwa Siku ya Mwaka Mpya wamekuja kwenye ulimwengu tofauti kabisa na mwaka mmoja uliopita." Kwa mustakabali wa watoto hawa, ametaka jamii ya kimataifa kufanya kazi pamoja akisema, "ufanye mwaka 2021 uwe aina ya Mwaka wa haki zaidi, salama na afya kwa watoto." 

Pia mwaka 2021 ni kumbukumbu ya miaka 75 tangu kuanzishwa kwa UNICEF.  

Katika kipindi cha mwaka mzima, UNICEF itafanya shughuli kadhaa za kumbukumbu na wadau wake, wakati ikiendelea kulinda watoto kutoka kwenye mizozo, magonjwa na kutengwa, na pia kuhakikisha inawatetea.  

Fowler ameongeza kusema, "wakati ulimwengu unakabiliwa na janga jipya la corona, kushuka kwa uchumi, kuongezeka kwa umaskini, na kuongezeka kwa ukosefu wa usawa, kazi ya UNICEF ni muhimu zaidi kuliko hapo awali. Katika miaka 75 iliyopita, iwe ni mizozo, makazi yao, majanga ya asili au katika majanga mengine, UNICEF imekuwa ikitoa msaada kwa watoto kote ulimwenguni. Katika mwaka huu mpya, tunaahidi tena kulinda usalama wa watoto na kusemea haki zao ili sauti zao zisikike bila kujali wanaishi wapi."