Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nalaani vikali shambulio uwanja wa ndege wa Aden Yemen:Griffiths

Martin Griffiths,Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mzozo wa Yemen.
UN Geneva/Violaine Martin
Martin Griffiths,Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu mzozo wa Yemen.

Nalaani vikali shambulio uwanja wa ndege wa Aden Yemen:Griffiths

Amani na Usalama

Mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Martin Griffiths amelaani vikali shambulio kwenye uwanja wa nderge wa Aden nchini Yemen lililotokea mapema leo.

Kupitia taarifa iliyotolewa muda mfupi baada ya shambulio hilo mwakilishi huyo amesema raia wengi wasio na hatia wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa katika shambulio hilo lililotokea muda mfupi baada ya kuwasili ndege iliyokuwa imebeba baraza la mawaziri la serikali mpya.

Bwaba. Griffiths ametuma salama za rambirambi na mshikamano kwa wote waliopoteza maisha na familia zao.

Pia amelitakia baraza hilo nguvu ya kuweza kukabiliana na jukumu gumu lililo mbele yao na kusistiza kwamba“Vitendo hivi vya machafuko havikubaliki n ani mkasa unaokumbusha umuhimu wa kuirejesha haraka Yemen katika njia ya kuelekea amani.”

Kwa mujibu wa duru mbalimbali za Habari takribani watu 16 wamekufa katika shambulio hilo na wengine 60 kujeruhiwa, lakini hakuna taarifa za yeyote kujeruhiwa kwa wale waliokuwa ndani ya ndege japo idadi ya vifo na majeruhi huenda ikaongezeka.