Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Wanafunzi wa Mauritania waliporejea shuleni baada ya miezi kadhaa ya shule kufungwa kutokana na COVID-19

Virusi vilivyoufunga ulimwengu: Elimu katika janga

© UNICEF/Raphael Pouget
Wanafunzi wa Mauritania waliporejea shuleni baada ya miezi kadhaa ya shule kufungwa kutokana na COVID-19

Virusi vilivyoufunga ulimwengu: Elimu katika janga

Afya

Watoto ulimwenguni kote masomo yao yamevurugika sana mwaka huu, kwani shule zinajitahidi kukabiliana na hali ya kufungwa na kufunguliwa tena kwa shule, na kuelekea katika masomo ya mtandaoni ikiwa hata ni chaguo. Watoto walio katika hali duni, hata hivyo, wameathirika zaidi na hatua za dharura zilizochukuliwa. Katika sehemu ya tatu ya tathimini yetu ya athari ya COVID-19 kwa ulimwengu, tunajikita kwenye janga la elimu lililosababishwa na janga la COVID-19.

Athari zisizo na kifani

Watoto katika eneo la Odisha India wakijifunza katika eneo la wazi kama tahadhari dhidi ya COVID-19.
UNICEF India
Watoto katika eneo la Odisha India wakijifunza katika eneo la wazi kama tahadhari dhidi ya COVID-19.

 

Kufungwa kwa shule kama matokeo ya janga la afya na majanga mengine sio mpya, angalau sio katika nchi zinazoendelea, na matokeo mabaya yanafahamika vizuri; kupoteza masomo na viwango vya juu vya kuacha masomo, kuongezeka kwa unyanyasaji dhidi ya watoto, mimba za utotoni na ndoa za mapema.
Kinachotofautisha janga la COVID-19 majanga mengine yote ni kwamba, COVID-19 imeathiri watoto kila mahali na kwa wakati mmoja.

Ni watoto maskini zaidi, walio katika mazingira magumu zaidi ambao wanaumizwa zaidi wakati shule zinapofungwa na kwa hivyo Umoja wa Mataifa kwa haraka ulifanya kutetea mwendelezo wa masomo, na ikiwezekana kufunguliwa salama kwa shule, wakati nchi zilipoanza kuweka hatua za kuzuia kukutembea: "kwa bahati mbaya, kiwango na kasi ya usumbufu wa kielimu duniani hakina kifani na ikiwa itaendelea, inaweza kutishia haki ya elimu.” Mwezi Machi, alionya Audrey Azoulay, Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO.  


Mgawanyiko kidijitali

 

Angures Buba, mwenye umri wa miaka 14 akitafuta masafa ya matangazo ya elimu ya darasa la 8 kwa njia ya redio. Hapa ni kwenye mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba na masomo anayosubiria kwa hamu ni Sayansi na Kiingereza.
© UNICEF/Helene Sandbu Ryeng
Angures Buba, mwenye umri wa miaka 14 akitafuta masafa ya matangazo ya elimu ya darasa la 8 kwa njia ya redio. Hapa ni kwenye mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba na masomo anayosubiria kwa hamu ni Sayansi na Kiingereza.

Wanafunzi na walimu walijikuta wakikabiliana na teknolojia isiyo ya kawaida ya mikutano, uzoefu ambao wengi waliona kuwa mgumu kuuzoea, lakini ambao ulikuwa njia pekee, kwa wengi wanaoishi katika hali ya kufungwa kwa mipaka, ya kuhakikisha aina yoyote ya elimu inaweza kuendelea.

Hata hivyo, kwa mamilioni ya watoto, wazo la kuhudhuria darasani kwa njia ya mtandao ni ndoto isiyofikika. Mwezi April, ilionesha mgawanyiko wa kidijitali ukionesha kuwa takribani watoto milioni 830 hawana kompyuta.

Picha ni mbaya katika nchi za kipato cha chini: takribani asilimia 90 ya wanafunzi katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara hawana kompyuta nyumbani, wakati asilimia 82 hawawezi kuingia  mtandaoni.

“Janga la kujifunza tayari lilikuwepo hata kabla ya COVID-19. Sasa tunaangalia mgogoro wa elimu unaogawanya na kuzidisha zaidi janga la kielimu.” Alisema afisa mmoja wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF mnamo mwezi Juni. 

Hata hivyo katika nchi zinazoendelea ambako kujifunza mtandaoni au kompyuta siyo chaguo kwa wanafunzi wengi, redio bado ina nguvu kuwafikia mamilioni ya wat una inatumika kuendeleza aina fulani ya elimu.

Sudan Kusini, Redio Miraya, inayotegemewa kwa habari za uhakika, chini ya usimamizi wa UNMISS, ilianza kurusha matangazo ya kielimu kwa watoto wengi ambao kutokana na hatua za COVID-19, walishindwa kuwa darasani. Unaweza kusikiliza ujumbe kutoka katika vipindi vya redio Miraya kutoka katika podcast kwa jina The Lid Is On. 


https://soundcloud.com/unradio/podcast-using-radio-as-a-powerful-teachi…


Je, ni kizazi kilichopotea?

Mtoto mwenye umri wa miaka 7 akisoma kwa njia ya mtandao huko Kyiv, Ukraine, wakati shule zikiendelea kufungwa kutokana na COVID-19.
©UNICEF/Filippov
Mtoto mwenye umri wa miaka 7 akisoma kwa njia ya mtandao huko Kyiv, Ukraine, wakati shule zikiendelea kufungwa kutokana na COVID-19.


Pamoja na juhudi hizo, Umoja wa Mataifa, mnamo mwezi Agosti ulikuwa unaonya kuwa madhara ya muda mrefu ya elimu iliyovurugwa yanaweza kutengeneza “kizazi kilichopotea” cha watoto barani Afrika. Utafiti wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO katika nchi 39 za kusini mwa Jangwa la Sahara ulionesha kuwa shule zilikuwa zimefunguliwa katika mataifa 6 pekee na kufunguliwa kwa kiasi fulani katika nchi 19. 


Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka, watoto milioni 320 walikuwa bado wamefungiwa nje ya shule duniani kote, na UNICEF ililazimika kutoa wito kwa serikali kuweka kipaumbele katika kuzifungua shule na kufanya madarasa kuwa salama iwezekanavyo.


"Kile ambacho tumejifunza kuhusu kusoma wakati wa COVID ni wazi: faida za kufungua shule, zinazidi gharama za kuzifunga, na kufungwa kwa shule kote kunapaswa kuepukwa kwa gharama yoyote." Anasema Robert Jenkins, Mkuu wa UNICEF.


Pamoja na kuwa ulimwengu unashuhudia ongezeko la COVID-19, na chanjo bado haziwezi kufikiwa na watu wengi, sera zaidi zilizo sawa zinahitajika kutoka kwa mamlaka ya kitaifa, badala ya kufunga kila kitu, anasema Bwana Jenkins. 


Bwana Yenkins ananukuliwa akisema, “ushahidi unaonesha kuwa shule sio sababu kuu za janga hili. Lakini tunaona hali ya kutisha ambayo serikali kwa mara nyingine tena zinafunga shule kama njia ya kwanza badala ya suluhisho la mwisho. Katika visa vingine, hii inafanywa nchi nzima, badala ya jamii na jamii, na watoto wanaendelea kupata athari mbaya katika kujifunza kwao, ustawi wa akili na mwili na usalama”.


SAUTI: 

MASOMO KWA NJIA YA REDIO: https://news.un.org/en/audio/2020/06/1066042
APP YA ELIMU AFGHANISTAN: https://news.un.org/en/audio/2020/07/1068001