Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres asihi uchaguzi uwe wa amani CAR baada ya walinda amani kutoka Burundi kuuawa

Afisa wa uchaguzi akitoa kadi ya kupigia kura kabla ya uchaguzi mkuu wa CAR utakaofanyika 27 Desemba 2020
MINUSCA/Hervé Serefio
Afisa wa uchaguzi akitoa kadi ya kupigia kura kabla ya uchaguzi mkuu wa CAR utakaofanyika 27 Desemba 2020

Guterres asihi uchaguzi uwe wa amani CAR baada ya walinda amani kutoka Burundi kuuawa

Amani na Usalama

Katika mkesha wa uchaguzi mkuu nchini Jamhuri ya Agfrika ya Kati CAR, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito kwa wadau wote kuhakikisha uchaguzi wa kesho Jumapili unafanyika kwa njia ya amani, uwe jumuishina wa kuaminika.

Katika taarifa iliyotolewa na msemaji wake hii leo Antonio Guterres amewataka wahusika wote wa uchaguzi huo kutoka pande zote“Kujizuia na vitendo vyoyote vitakavyotia dosari uchaguzi huo ikiwemo machafuko, kauli za chuki na uchochezo wa machafuko ambavyo vitatishia maisha ya wat una kutia dosari mchakato mzima wa uchaguzi na utulivu wa kitaifa.”

Bwana Guterres pia ametoa wito kwa wadau wote wa kisiasa na wafuasi wao”Kutatua tofauti zao kwa njia ya amani, ikiwemo kupitia majadiliano na mfumo unaotambulika wa taasisi za kitaifa kwa kuzingatia sheria za kitaifa.”

Walindamani wa MINUSCA wakifanya doroa katika mji mkuu wa CAR Bangui mwaka 2017.
UN Photo/Herve Serefio
Walindamani wa MINUSCA wakifanya doroa katika mji mkuu wa CAR Bangui mwaka 2017.

Wimbi la machafuko

Nchi ya CAR inapiga kura kesho tarehe 27 Desemba huku kukiwa na wimbi kubwa la ongezeko la machafuko.

Ijumaa walindamani wa mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MINUSCA na vikosi vya usalama vya kitaifa walishambuliwa na watu wenye silaha wasiojulikana katika eneo la Kati na Kusini mwa nchi hiyo. Na katika shambulio hilo walindaamani 3 kutoka Burundi waliuawa na wengine wawili kujeruhiwa.

Pia kumekuwa na ongezeko la kasi la machafuko dhidi ya wahudumu wa kibinadamu, raia, mamlaka za serikali Pamoja na wagombea.

Msaada na mshikamano

Katika taarifa hiyo Katibu Mkuu amelaani vikali mashambulizi hayo na kutoa wito kwa mamlaka ya CAR kuhakikisha uwajibikaji kwa machafuko yote yanayohusiana na uchaguzi.

“Amezitaka pande zote zilizotia Saini makubaliano ya kisiasa ya amani na maridhiano nchini CAR kuzingatia ahadi zao katika mkataba huo na kushughulikia malalamiko yao kwa njia ya amani.”

Bwana Guterres pia amerejea kuwahakikishia watu wa CAR kuenfdfelea kwa msaada na mshikamano wa Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na uratibu wa wadai wa kitaifa, kikanda na kimataifa, wakati wakipambana kurejesha amani na demokrasia katika nchi yao.