Nalaani vikali mauaji ya watu 27 na kuchomwa kwa nyumba 800 Niger:Guterres 

Eneo la Diffa nchini Niger
UNICEF/ Cherkaoui
Eneo la Diffa nchini Niger

Nalaani vikali mauaji ya watu 27 na kuchomwa kwa nyumba 800 Niger:Guterres 

Masuala ya UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali shambulio lililofanywa na watu wenye silaha wasiojulikana kwenye jimbo la Diffa nchini Niger. 

Akijibu swali kuhusu shambulio hilo kwenye mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika kwa njia ya mtandao hii leo mjini New York Marekani , msemaji wa Katibu Mkuu amesema shambulio hilo lilifanyika Desemba 12 na kukatili watu 27 na nyumba 800 zikiripotiwa kuchomwa moto. 

Ameongeza kuwa Katibu Mkuu ametuma salamu za rambirambi kwa familia zilizopoteza wapendwa wao, wat una serikali ya Niger na kuwatakia ahuweni ya haraka majeruhi wote. 

Bwana. Guterres amesema amesikitishwa kwamba shambulio hilo la kikatili limevuruga kufanyika kwa amani kwa uchaguzi wa manispaa na wa kanda kwenye jimbo la Diffa. 

Amerejea kusisitiza ahadi ya Umoja wa Mataifa ya kusaidia juhudi za serikali ya Niger za kuwa na utawala wa kidemokrasia, kuchagiza mahusiano ya kijamii na kufikia malengo ya maendeleo endelevu SDG’s.