Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada wa nchi tajiri kwa watoto wakati wa COVID-19 hautoshi:UN Ripoti 

WFP imesambaza chakula kwa jamii masikini Gaza kwa kutumia vocha za kielektroniki kw aajili ya kupata bidhaa muhimu.
WFP/Wissam Nassar
WFP imesambaza chakula kwa jamii masikini Gaza kwa kutumia vocha za kielektroniki kw aajili ya kupata bidhaa muhimu.

Msaada wa nchi tajiri kwa watoto wakati wa COVID-19 hautoshi:UN Ripoti 

Msaada wa Kibinadamu

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF limekosoa kiwango cha msaada wa kifedha uliotengwa kwa ajili ya kusaidia watoto katika nchi tajiri wakati huu wa janga la corona au COVID-19 na kusema hakitoshi. 

Ripoti ya shirika hilo ya umasikini kwa watoto iliyotolewa leo imesema kati yad ola trilioni 14.9 zinazotumika kwa ajili ya mikakati yua kujikwamua na COVID-19 kwenye nchi tajiri ni asilimia 2 tu ya fedha hizo ndizo zilizotengwa kwa ajili ya watoto na familia zinazolea watoto. 

Ripoti hiyo imesema na hali hii inatokea licha ya Ushahidi kwamba umasikini unatarajiwa kusalia katika kiwango cha juu zaidi ya ilivyokuwa kabla ya COVID-19 kwa angalau miaka mitano katika nchi za kipato cha juu. 

“Kiwango cha fedha za msaada kilichotengwa moja kwa moja kwa Watoto na familia hakiendani na athari kubwa za janga hili la COVID-19 na kwa muda ambao janga hili linatarajiwa kuathri nchi hizo” amesema Gunila Olsson mkurugenzi wa UNICEF ofisi ya utafiti Innocenti Florence Italia. 

WFP inasaidia akina mama kutoka Palestina kulea watoto wao kwa afya licha ya mazingira ya umasikini na madhila.
WFP
WFP inasaidia akina mama kutoka Palestina kulea watoto wao kwa afya licha ya mazingira ya umasikini na madhila.

Makampuni ndio washindi 

Ripoti hiyo imebaini kwamba makampuni ya biashara ndio wafaidika wakubwa wa fedha hizo za msaada wa kujikwamua ambapo asilimia karibu 80 ya fedha hizo zinakwenda kwao na kwa mantiki hiyo watoto wengi kutoka makundi ya pembezoni au yasiyojiweza ndio watakaoathirika zaidi. 

Ripoti imeongeza kuwa theluthi ya nchi hizo zenye uchumi mkubwa zilizofanyiwa utafiti katika ripoti hii kutoka nchi za Muungano wa Ulaya na nchi zingine zenye kipato cha juu hawakutekeleza sera zozote maalum zilizolenga kusaidia watoto wakati wa wimbi la kwanza la COVID-19. 

Pia ripoti inasema kwa ujumla hatua za ulinzi wa hifadhi ya jamii kwa watoto na familia ambazo baadhi ya nchi hizo ilizichukua kama vile huduma ya ulezi wa watoto, shule na msaada wa fedha kwa familia zilidumu tu kwa miezi mitatu ikiwa ni muda mfupi sana kuweza kushughulikia matarajio ya muda mrefu ya janga hilo na hatari za umasikini kwa watoto kwa muda mrefu. 

Wakati huu ambapo msimu wa baridi umeingia katika sehemu mbalimbali duniani na wagonjwa wa COVID-19 kuongezeka UNICEF imeitaka serikali kuweka mikakati yenye uwiano zaidi katika kujikwamua na janga la COVID-19 katika wakati huu ambao Unaitwa ni wa wimbi la pili za COVID-19” na kutilia mkazo ulinzi wa hifadhi ya jamii kwa Watoto na kuwa na msaada usio na masharti kwa familia masikini , fedha kwa ajili ya chakula, kutoa huduma za malezi ya watoto, kulipia Ankara na kodi ya pango au mikopo ya nyumba.