Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki za binadamu lazima ziwe 'mbele na katikati' ya mapambano dhidi ya COVID-19-Katibu Mkuu UN 

Madarasa nchini Egypt vinasafishwa na kupigwa na dawa maalum ya kuzuia kuzambaa vya COVID-19
© UNICEF/Ahmed Mostafa
Madarasa nchini Egypt vinasafishwa na kupigwa na dawa maalum ya kuzuia kuzambaa vya COVID-19

Haki za binadamu lazima ziwe 'mbele na katikati' ya mapambano dhidi ya COVID-19-Katibu Mkuu UN 

Haki za binadamu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito wa haki za binadamu kuwekwa "mbele na katikati" ya mapambano na kupona dhidi ya COVID-19 ulimwenguni kote ili kufanikisha maisha bora ya baadaye kwa watu kila mahali. 

Bwana Guterres, ametoa ombi hilo katika ujumbe wake kwa Siku ya Haki za Binadamu, ambayo imeadhimishwa hii leo Alhamisi. 

 “Watu na haki zao lazima ziwe mbele na katikati mwa kupambana na kupona. Tunahitaji mifumo ya ulimwengu inayotegemea haki kama vile chanjo ya afya kwa wote, ili kushinda janga hili na kutulinda kwa siku zijazo.” Amesema Guterres.  

Ukiukaji ulituumiza sisi sote 

Janga hilo la COVID-19 limeimarisha ukweli wa kimsingi kuhusu haki za binadamu, amesema Katibu Mkuu, akianza na mtazamo kwamba, “ukiukaji unatudhuru sisi sote.” 

"Janga la COVID-19 limekuwa na athari kubwa kwa makundi ya watu walioko hatarini ikiwa ni pamoja na wafanyakazi waliko mstari wa mbele, watu wenye ulemavu, wazee, wanawake na wasichana, na jamii za wachache. Imefanikiwa kwa sababu umasikini, ukosefu wa usawa, ubaguzi, uharibifu wa mazingira yetu ya asili na ukosefu mwingine wa haki za binadamu, vimeunda udhaifu mkubwa katika jamii zetu. Wakati huo huo, janga hilo linadhoofisha haki za binadamu, kwa kutoa kisingizio cha hatua nzito za kiusalama na hatua za kali ambazo zinapunguza nafasi ya raia na uhuru wa vyombo vya habari. "” Amesema Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa.  

Mgawanyiko haufanyi kazi 

Aidha Bwana Guterres kupitia ujumbe wake huo kuhusu siku ya kimataifa ya haki za binadamu amesema ukweli wa pili ni kwamba haki za binadamu ni za ulimwengu wote na zinamlinda kila mtu, hali hiyo ikisisitiza jinsi athari ya janga inapaswa kuwa msingi wa mshikamano na ushirikiano. 

"Mbinu za mgawanyiko, ubabe na utaifa hauna maana yoyote dhidi ya tishio la ulimwengu." Amesisitiza.   

Kabla tu ya janga la virusi vya corona, Katibu Mkuu Guterres alitoa wito wake kwa Hatua ya Haki za Binadamu. Wito huo ukielezwa kama miongozo saba ya mabadiliko chanya, unaeleza jukumu kuu la haki za binadamu katika maeneo kama vile kukabiliana na janga, usawa wa kijinsia, ushiriki wa umma na maendeleo endelevu.   

Guterres pia amesema, "katika Siku ya Haki za Binadamu na kila siku, tuamue kuchukua hatua kwa pamoja, na haki za binadamu mbele na katikati, kupona kutoka dhidi ya janga la COVID-19 na kujenga maisha bora ya baadaye kwa wote."