Dunia inapaswa kutumia utajiri wake kuzuia baa la njaa-WFP 

David Beasley, Mkurugenzi mtendaji wa WFP akiwa na tuzo ya Nobel kwa niaba ya shirika lake mshindi wa tuzo hiyo mwaka 2020.
© WFP/Rein Skullerud
David Beasley, Mkurugenzi mtendaji wa WFP akiwa na tuzo ya Nobel kwa niaba ya shirika lake mshindi wa tuzo hiyo mwaka 2020.

Dunia inapaswa kutumia utajiri wake kuzuia baa la njaa-WFP 

Msaada wa Kibinadamu

Mkurugenzi mtendaji wa shirika la mpango wa chkula la Umoja wa Mataifa WFP David Beasly ameiasa dunia kutumia utariji wake kuhakikisha inazuia baa la njaa duniani wakati akipokea rasmi tuzo ya amani ya Nobel ambayo shirika hilo lilitangazwa kushinda mwezi Oktoba.

Bwana Beasley ambaye amekabidhiwa rasmi tuzo hiyo kwenye hafla maalum katika makao makuu ya WFP mjini Roma Italia hii leo amesema “Kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, bodi yetu, mashirika wadau na wahisani na muhimu zaidi wafanyakazi  zaidi ya 19,000 wa WFP na wengine wote waliotutangulia waliopoteza maisha wakihudumu Pamoja na familia zao, na kwa niaba ya watu milioni 100 wenye njaa duniani , kwenda kwa kamati ya amani ya Nobel ya Norway asante sana kwa heshma hii kubwa.”  

Juvenal Kisanga ni miongoni mwa wafanyakazi wa WFP ambaye ni afisa programu mwandamizi wa shirika hilo nchini Tanzania akizungumzia tuzo hiyo amesema 

Bwana. Beasley amesisitiza kwamba kushindwa kuzuia baa la njaa sasa kutasambaratisha maisha ya mamilioni ya watu na kusababisha kuanguka kwa kile ambacho dunia nzima inakikumbatia amani, kwani anaamini kwamba chakula ni njia ya kuelekea amani. 

Kwa mantiki hiyo amesema tuzo hii ni zaidi ya asante ya kazi kubwa ya WFP bali ni wito wa kuchukua hatua kwa sababu dunia hivi sasa imeghubikwa na vita, mabadiliko ya tabia, matumizi ya njaa kama silahaza ya kisiasa na kijeshi na sasa janga la COVID-19 ambalo limefanya hali kuwa mbaya zaidi kwani watu milioni 270 wengine kote duniani wanaelekea kutumbukia katika njaa na kati yao milioni 30 wanaitegemea WFP kwa msaada wa asilimia 100.