Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kupungua kwa hewa chafuzi angani kunaweza kusaidia kufikia lengo la chini ya nyuzi joto 2 za Selisiasi-UNEP 

Moshi kutoka kwa nyumba ya kuoka mikate inayotumia mkaa.
UNICEF/Shehzad Noorani
Moshi kutoka kwa nyumba ya kuoka mikate inayotumia mkaa.

Kupungua kwa hewa chafuzi angani kunaweza kusaidia kufikia lengo la chini ya nyuzi joto 2 za Selisiasi-UNEP 

Tabianchi na mazingira

Janga la uchafuzi wa hali ya hewa linaweza kupungua hadi asilimia 25 kwenye uzalishaji wa hewa chafuzi uliotabiriwa kufikia mwaka 2030 na hivyo kuileta dunia karibu kufikia lengo la nyuzi joto 2 kipimo cha selisiasi za Mkataba wa Paris, imeeleza ripoti mpya ya shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP.   

Ripoti hiyo ya mwaka 2020 ya UNEP ya pengo la uzalishaji wa hewa chafuzi, imegundua kuwa, licha ya kupungua kwa uzalishaji wa hewa ukaa kwa 2020 uliosababishwa na janga la COVID-19, ulimwengu bado unaelekea kuongezeka kwa joto zaidi ya nyuzi joto 3 selisiasi katika karne hii. 

Hata hivyo, ikiwa serikali zitawekeza katika hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kama sehemu kupona kutoka katika janga la uchafuzi wa hali ya hewa, na kuimarisha ahadi katika mkutano ujao wa hali ya hewa unaofanyika Glasgow mwezi Novemba 2021 ili ziweze kufikisha lengo la uzalishaji wa hewa chafuzi kwa viwango vilivyo sawa na nyuzijoto 2 za selisiasi. 

Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP anasema, "mwaka wa 2020 unaelekea kuwa moja ya miaka yenye joto zaidi kwenye rekodi, wakati moto wa porini, dhoruba na ukame unaendelea kusababisha maafa. Hata hivyo, ripoti ya pengo la uzalishaji wa hewa chafuzi inaonesha kuwa ahueni ya janga la uchafuzi wa hali ya hewa linaweza kumega kipande kikubwa kutoka kwenye uzalishaji wa hewa chafuzi na  kusaidia kupunguza kasi ya mabadiliko ya hali ya hewa. Ninasihi serikali kuunga mkono hali hii  katika hatua inayofuata ya kupambana na COVID-19 na kuongeza kwa kiasi kikubwa matarajio yao ya tabianchi kwa mwaka 2021.” 

Kila mwaka, ripoti ya pengo la uzalishaji wa hewa chafuzi hutathmini pengo kati ya uzalishaji unaotarajiwa na viwango vinavyoendana na malengo ya Mkataba wa Paris ya kupunguza ongezeko la joto ulimwenguni karne hii hadi chini ya nyuzijoto 2 za selisiasi na kufikia nyuzijoto 1.5 za selisiasi. Ripoti hiyo inagundua kuwa katika mwaka 2019 jumla ya uzalishaji wa hwa chafuzi, pamoja na mabadiliko ya matumizi ya ardhi, ilifikia kiwango kipya cha mabilioni ya tani 59.1 za hewa chafuzi, GtCO2e. Uzalishaji wa hewa chafuzi duniani umekua kwa asilimia 1.4 kwa mwaka tangu 2010 kwa wastani, na ongezeko la haraka zaidi la asilimia 2.6 mnamo 2019 kwa sababu ya ongezeko kubwa la moto wa misitu. 

Matokeo ya kupungua kusafiri, shughuli za viwandani kuwa chini na uzalishaji mdogo wa umeme mwaka huu kwa sababu ya janga la corona, uzalishaji wa hewa chafuzi unatabiriwa kushuka hadi asilimia 7 katika mwaka huu wa 2020. Hata hivyo, kupungua huku kunatafsiriwa tu kuwa punguzo la nyuzi joto 0.01 za selisiasi katika ongezeko la joto ulimwenguni  ifikapo mwaka 2050.  

Kubadilisha tabia ya matumizi ni muhimu 

Kila mwaka ripoti hii pia inaangalia kuhusu mchango wa sekta maalum. Kwa mwaka huu wa 2020 imezingatia tabia za watumiaji na pia sekta za usafirishaji wa majini na angani.  

Sekta hizi mbili, ambazo zinachangia asilimia 5 katika uzalishaji wa hewa chafuzi, pia zinahitaji kuangaliwa. Uboreshaji wa teknolojia na shughuli zinaweza kuongeza ufanisi wa nishati, lakini ongezeko la makadirio ya mahitaji linamaanisha hii haitasababisha upunguzaji wa uchafuzi  na upunguaji kamili wa hewa ukaa. Sekta zote mbili zinahitaji kuchanganya ufanisi wa nishati na mabadiliko ya haraka mbali na mafuta ya kisukuku, ripoti imeeleza. 

Ripoti hiyo imebaini kuwa hatua kali dhidi ya tabianchi lazima zijumuishe mabadiliko katika tabia ya matumizi na sekta binafsi na watu binafsi. Karibu theluthi mbili ya uzalishaji wa hewa chafuzi  ulimwenguni inahusishwa na  matumizi katika kaya binafsi.