Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali ya kibinadamu Tigray bado ni tata mno, wasiwasi ni mkubwa-UN 

Mkimbizi kutoka Tigray akisubiri mgao wa chakula makazi ya Um Rakuba nchini Sudan.
WFP/Arete/Joost Bastmeijer
Mkimbizi kutoka Tigray akisubiri mgao wa chakula makazi ya Um Rakuba nchini Sudan.

Hali ya kibinadamu Tigray bado ni tata mno, wasiwasi ni mkubwa-UN 

Amani na Usalama

Mkurugenzi wa Huduma ya Habari ya Umoja wa Mataifa Alessandra Vellucci, akijibu maswali ya wanahabari hii leo mjini Geneva Uswisi, amesema kwamba Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ana wasiwasi kuhusu hali ya sasa katika mkoa wa Tigray nchini Ethiopia. 

Alessandra Vellucci ameyaeleza hayo akiwa ameongoza mkutano wa wanahaari uliohudhuriwa na wasemaji na wawakilishi wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na uratibu wa misaada ya kibinadamu, OCHA, Mpango wa Chakula Ulimwenguni, WFP, Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR,  Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Jumuiya ya Utangazaji ya Ulaya. 

Bwana Vellucci ameeleza kuwa, “Katibu Mkuu Guterres anahisi kuwa ni muhimu kurudisha haraka utawala wa sheria, kwa heshima kamili ya haki za binadamu, kukuza mshikamano wa kijamii, upatanisho uliojumuishwa, na vilevile kuanzisha tena utoaji wa huduma za umma na kuhakikisha ufikiaji wa misaada ya kibinadamu bila kizuizi. Umoja wa Mataifa unaendelea kujitolea kabisa kuunga mkono mpango wa Muungano wa Afrika.” 

Kwa upande wake Jens Laerke, Msemaji wa OCHA, akijibu swali kuhusu tukio linalodaiwa kuwahusisha wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa huko Tigray, lakini kwa usalama wa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa waliko katika eneo hilo,  kwa sasa  hakuna maoni yanayoweza kutolewa kuhusu suala hili.  

Na Msemaji wa UNHCR, Babar Baloch, kwa upande wao, ameeleza kuwa hali ya kibinadamu inazidi kuwa mbaya. Kanuni za ubinadamu, usawa, kutopendelea na uhuru wa kufanya kazi zinahitajika kutekelezwa.  

“Cha kusikitisha, upatikanaji wa misaada ya kibinadamu bado haukuwezekana na hakukuwa na habari za zinazoendana na wakati kwa mwezi mmoja sasa. UNHCR inabaki na wasiwasi sana kwa usalama wa wakimbizi huko Tigray. Ukosefu wa ufikiaji watu unaamaanisha kuwa wakimbizi na wengine wenye uhitaji, hawawezi kufikiwa. UNHCR bado inatumia idadi ya wakimbizi 96,000 wa Eritrea katika mkoa huo ambao hawakuweza kupatikana.” Amesema Babar Baloch.   

Aidha Baloch ameongeza kuwa wakati huo huo, wakati wakimbizi wa Ethiopia waliendelea kuwasili Sudan, idadi ya waliowasili imekuwa ikipungua, na imesimamia kwenye 400-600 kwa siku. Wakimbizi wamekuwa wakiripoti kuongezeka kwa vituo vya ukaguzi njiani. Hadi hivi sasa, zaidi ya watu 49,000 wamesajiliwa kuvuka kutoka Ethiopia kuingia Sudan.