Bangi sasa si uraibu haramu na hatari  kutokana na faida za kiafya:WHO 

3 Disemba 2020

Kufuatia mapendekezo ya shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO ya faida za kitabibu zinazotokana na zao la bangi kwa afya , nchi 27 wanachama wa tume ya Umoja wa Mataifa ya dawa za kulevya wamepiga kura kuunga mkono kuondoa bangi katika orodha ya dawa hatari za kulevya katika maamuzi ambayo pia yalipingwa kwa kura 25 na mjumbe mmoja kutopiga kura. 

Tume hiyo ya Umoja wa Mataifa ya dawa za kulevya imeitoa bangi katika orodha ya dawa hatari za kulevywa ikiongoza mabadiliko ambayo sasa yanatokea kimataifa kuhusu matumizi ya bangi. 

Ikitathimini mlolongo wa mapendekezo ya WHO kuhusu bangi au marijuana na athari zake tume hiyo imejikita katika kuondoa bidhaa hiyo kwenye orodha namba IV ya mkataba kuhusu dawa za kulevya wa mwaka 1961 ambao uliiorodhesha bango sambamba na dawa zingine hatari za kulevya kama heroine. 

Nchi zote 53 wanachama wa tume hiyo zimepiga kura ya kuiondoa bangi katika orodha iliyodhibiti matumizi yake kwa miaka 59 yakiwemo matumizi ya kitabibu. 

Kwa matokeo hayo ya kihistoria ya kura 27 kuunga mkono, 25 kupinga na mwanachama mmoja kutopiga kura , tume hiyo ya Umoja wa Mataifa imefungua mlango wa kutambua uwezekano wa matumizi ya kawaida ya kimatibabu ya bidhaa za bangi ambazo bado sehemu nyingi duniani matumizi yake ni haram una kinyume cha sheria. 

Kwa mujibu a duru mbalimbali za Habari maamuzi hayo yanaweza kuwa kichocheo cha utafiti zaidi kuhusu masuala ya kitabibu ya mmea huo na pia kutumika kama chachu kwa nchi zkuhalalisha matumizi yake kwa matibabu na kufikiria pia kuwa na sheria za kuruhusu matumizi ya burudani ya bidhaa za bangi. 

Mifereji ya kuvutia bangi ikiuzwa mjini New York, Marekani
UN News/Elizabeth Scaffidi
Mifereji ya kuvutia bangi ikiuzwa mjini New York, Marekani

Subira yavuta heri 

Januari mwaka 2019 WHO ilitoa mapendekezo sita yanayohisana na matumizi ya bangi na kutana itolewe kwenye orodha ya mikataba ya Umoja wa Mataifa ya kudhibiti dawa za kulevya. 

Tume ya Umoja wa Mataifa ya kudhibiti dawa za kulevya mwanzo ilipiga kura kuhusu mapendekezo hayo ya WHO katika kikao chake cha mwezi Machi mwaka janaambapo nchi nyingi ziliomba muda zaidi wa kutafakari kuhusu kuunga mkono kutolewa kwa bangi kwenye orodha ya dawa hatari za kulevya na pia kuweza kuweka bayana misimamo yao kuhusu suala hilo zimesema duru mbalimbali za Habari. 

Miongoni mwa mambo ambayo WHO iliyachapisha kuhusu bangi ni kufafanua kwamba kuna baadhi ya sehemu ya mmea huo wa bangi iitwayo cannabidiol (CBD) ambayo haileweshi haipaswi kudhibitiwa kimataifa hasa kwa sababu imeanza juku muhimu la kile kinachoitwa matumizi ya kiafya katika miaka ya karibuni huku sekta ya mabilioni yad ola ikiundwa. 

Hivi sasa nchi zaidi ya 50 duniani zimeanzisha program za matumizi ya kitabibu ya bangi, nchi nyingine kama Canada, Uruguay na majimbo 15 ya Marekani yamehalalisha matumizi ya burudani ya bangi. Na nchi kama Mexico na Luxembourg zitafanyia kazi uwezekano huo. 

Misimamo tofauti 

Baada ya kura kupigwa baadhi ya nchi zilitaka kutoa maelezo ya kura zao. Mathalan Ecuador ilisema inaunga mkono mapendekezo yote ya WHO na kwamba “katika nchi yake uzalishaji, uuzaji na matumizi ya bangi yana mfumo wa ufuatiliaji ambao utahakikisha matumizi mazuri, ubora, ubunifu na ufanyaji wa utafiti.” 

Wakati huohuo Marekani ambayo imepiga kura ya kutaka bangi iondolewe kwenye orodha ya IV ya mkataba wa kudhibito dawa za kulevya imlikuwa inataka bidhaa hiyo isalie kwenye orodha ya I ikidai kwamba “Ingawa inakubalia na sayansi kwamba sehemu ya mmea huo wa bangi imetengenezwa kuwa salama na kufanyakazi inayotakiwa kiafya, lakini bangi yenyewe bado ni toshio lenye hatari kubwa kwa afya ya umma na hivyo iendelee kudhibitiwa chini ya mikataba ya kimataifa ya udhibiti wa dawa za kulevya.” 

Nazo nchi nyingine kama Chile imekuwa ikipinga miongoni mwa mambo mengine ikisema kwamba “kuna uhusiano wa moja kwa moja baina ya matumizi ya bangi na ongezeko la uwezekano wa msongo wa mawazo, matatizo ya akili, shauku na hadili za uendawazimu”, huku Japani kwa upande wake ikisema kwamba matumizi ambayo sio ya kitabibu ya bangi   “Yanaweza kusababisha athari mbaya za kijamii na kiafya hususan miongoni mwa vijana.” 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter