Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi: Ni wakati wa kutengeneza amani na asili-Katibu Mkuu wa UN  

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akizungumza hali ya sayari dunia akiwa na Profesa Raymo chuo cha Columbia jijini New York.
UN Photo/Eskinder Debebe)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akizungumza hali ya sayari dunia akiwa na Profesa Raymo chuo cha Columbia jijini New York.

Hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi: Ni wakati wa kutengeneza amani na asili-Katibu Mkuu wa UN  

Masuala ya UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, ameelezea mapambano dhidi ya janga la mabadiliko ya tabianchi kama kipaumbele cha juu kwa karne ya 21, kupitia hotuba yake aliyoitoa Jumatano hii katika Chuo Kikuu cha Columbia mjini New York Marekani.  

Hotuba hiyo ya kihistoria inaashiria mwanzo wa mwezi wa hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi chini ya uongozi wa Umoja wa Mataifa, mwezi ambao unajumuisha kutolewa kwa ripoti kubwakubwa kuhusu tabianchi ya ulimwengu na uzalishaji wa mafuta ya kisukuku, na kukamilika katika mkutano wa tabianchi mnamo tarehe 12 Desemba, maadhimisho ya tano ya mkataba wa Paris wa mwaka 2015.  

Asili mara zote huwa inajibu mapigo 

Bwana Guterres amenaza hotuba yake kwa kuonesha njia nyingi ambazo asili inaitikia kwa nguvu inayoongezeka na ghadhabu kwa utunzaji mbayá mazingira unaofanywa na mawanadamu hali inayosababisha kupromoka kwa bionuai, kuenea kwa jangwa na baharí kufikia rekodi za juu za joto.  

Uhusiano kati ya COVID-19 na mabadiliko ya tabianchi yaliyotengenezwa na mwanadamu pia yamewekwa wazi na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye amebaini kuwa uvamizi wa watu na mifugo katika makazi ya wanyama, “kuna hatari ya kutuweka katika magonjwa hatari zaidi.” 

‘Wakati wa kubonyeza kitufe cha kijani kibichi’ 

Jibu linalofaa la ulimwengu, anasema Katibu Mkuu Guterres, kuwa ni mabadiliko ya uchumi wa ulimwengu, kubonyeza "kitufe cha kijani" na kujenga mfumo endelevu unaosababishwa na nishati mbadala, kazi za kijani na siku zijazo zenye mnepo.   

 “Njia moja ya kufikia maono haya, ni kwa kufanikisha uzalishaji sifuri wa hewa chafuzi. Kuna ishara za kutia moyo, na nchi kadhaa zilizoendelea, pamoja na Uingereza, Japani na Uchina, zinajitolea kufikia lengo katika miongo michache ijayo.” Amesema Bwana Guterres.