Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umewahi kusikia kuhusu mwanaharakati wa hisabati? 

Watoto wakiwa darasani nchini Sudan Kusini
UNICEF/Shehzad Noorani
Watoto wakiwa darasani nchini Sudan Kusini

Umewahi kusikia kuhusu mwanaharakati wa hisabati? 

Utamaduni na Elimu

Dunia inakuwa mahali bora pa kuishi ikiwa kila mtu atachangia katika kutaka hali hiyo itokee. Kutana na Yusuf Adamu Ibrahim, mwanaharakati mchanga wa hisabati kutoka jimbo la Bauchi, Nigeria ambaye anabadilisha maisha ya watoto wa shule katika jamii yake kwa kuwasaidia kuboresha ujuzi wao wa hesabu. Yusuf ni hamasa kwa wengi, na ni kijana mdogo wa umri wa miaka 18 mpenda mabadiliko.

Ni Yusuf Adamu Ibrahim mkazi wa Bauchi Nigeria. Kama anavojitambulisha ni mwanaharakati wa hisabati na ni kijana mdogo mwanafunzi wa kidato cha tatu. Unaharakati wake ni kuwasaidia wenzake katika kuboresha ujuzi wao wa hisabati na pia kuwafundisha watu wote katika jamii yake kuhusu hisabati.  

Mwanaharakati huyu wa hisababati mwenye umri wa miaka 18, anaonekana akiwafundisha vijana wenzake wadogo na watu wengine wazima wanafuatilia akiwemo baba yake mzazi. 

Baada ya muda mfupi akiwa amekaa katika chumba ambacho nyuma yake kumesheheni tuzo mbalimbali na vyeti alivyoshinda katika mashindano mbalimbali ya hisabati anasema, “ninachopenda kuwa mwanaharakati ni ukweli kuwa mwanaharakati anatoa kila alichonacho kwa faida ya watu. Ninafurahi kuwapa watu maarifa na uzoefu ambao nimeupata katika miaka ya maisha yangu ya kushindana na wengine kutoka katika majimbo mbalimbali na sehemu nyingine za nchi. Na hii imenipa uzoefu mzuri ambao ningependa kuwapa wengine.” 

Yusuf alivutiwa kwanza na baba yake ambaye naye ni mwanahisabati ambaye ndiye hasa alianza kuwasaidia vijana wengi katika eneo lao kupenda hisabati na hata baadhi yao kufikia kushirikia mashindano ya kitaifa na kimataifa. Yusuf anasema hatua hiyo ya a baba yake imechangia kumhamasisha kutaka naye kurejesha chochote kwa jamii. Na anatumaini  uanaharakati wake utapanda zaidi na kuendelea kutoka katika mazingira madogo ya jamii ndogo hadi mazingira ya jamii pana zaidi.  

Sasa ni muda wa kupumzika, kama yalivyo maisha ya vijana wadogo wenzake, Yusuf sasa anauchezea mpira na anasema, “mapenzi yangu ni kwa mpira wa miguu. Ninapenda kucheza mpira wa miguu katika muda wangu wa mapumziko. Pindi ambapo ninakuwa sina cha kufanya au ninapokuwa nimechoka na kusoma.”