Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vita dhidi ya COVID-19 vyaweza kujifunza kutoka kwenye mapambano dhidi ya HIV:Guterres 

Mwanamke anayeishi na ukimwi na mwanae wanakunywa dawa kila siku nyumbani kwao Mabarara, magharibi mwa Uganda.
© UNICEF/Karin Schermbrucker
Mwanamke anayeishi na ukimwi na mwanae wanakunywa dawa kila siku nyumbani kwao Mabarara, magharibi mwa Uganda.

Vita dhidi ya COVID-19 vyaweza kujifunza kutoka kwenye mapambano dhidi ya HIV:Guterres 

Afya

Wakati nguvu za dunia zikielekezwa katika janga la corona au COVID-19, siku ya ukimwi duniani ni kumbusho kwamba kuna haja ya kuendelea kutilia maanani janga lingine kubwa ambalo linaikabili dunia kwa karibu miaka 40 sasa tangu lilipozuka amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa. 

Antonio Guterres amesema hayo kupitia ujumbe wake maalum wa siku ya ukimwi duniani inayoadhimishwa kila mwaka Desema Mosi na kuongeza kuwa “licha ya mafanikio makubwa yaliyopatikana dharura ya gonjwa la ukimwi bado haijaisha. Watu milioni 1.7 wanaambukizwa virusi vya VVIU kila mwaka huku watu 690,000 wakipoteza maisha na pengo la kutokuwepo kwa usawa linamaanisha kwamba wale wasioweza kusimamia haki zao ndio wanaoathirika zaidi.” 

Amesisitiza kwamba janga la coronavirus">COVID-19 imekuwa ni kengeke ya kuiamsha dunia kwamba pengo la usawa katika masuala ya afya linatuathiri sote na hakun aliyekuwa salama hadi pale wote tutakapokuwa salama. 

Katibu Mkuu amesema vita dhidi ya VVU vina mengi ya kuyafundisha mmapambano dhidi ya COVID-19. 

Tunajua kwamba ili kutokomeza janga la ukimwi na COVID-19 ni lazima kumalize unyanyapaa na ubaguzi, tuwape watu kipaumbele nah atua zetu zijikite katika haki za binadamu na mitazamo inayokumbatia masuala ya kijinsia.” 

Bwana Guterres amesisitiza kwamba “Utajiri usiwe kigezo cha kuamua wendapo watu wapate huduma za afya wanazohitaji ama la. Tunahitaji chanjo ya COVID-19, matibabu ya VVU na huduma ambazo watu wanaweza kumudu na zinazopatikana kwa wote kila mahali.” 

Ameongeza kuwa afya ni haki ya binadamu na afya lazima iwe kipaumbele cha kwanza katika uwekezaji ili kuweza kufikia huduma za afya kwa wote. 

Katika siku hii ya ukimwi ameitaka dunia kutambua kwamba kutokomea janga la COVID-19 na kumaliza ukimwi lazima ishikamane na kubeba majukumu kwa pamoja.