Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ufadhili endelevu unahitajika kutopoteza mafanikio yaliyofikiwa katika vita dhidi ya VVU-Msichana Moraa

Doreen Moraa Moracha kutoka Kenya alizaliwa na Virusi Vya Ukimwi na hivi sasa anatumia mitandao ya kijamii kuelezea simulizi yake ya kupendeza juu ya maisha yake.
UN News
Doreen Moraa Moracha kutoka Kenya alizaliwa na Virusi Vya Ukimwi na hivi sasa anatumia mitandao ya kijamii kuelezea simulizi yake ya kupendeza juu ya maisha yake.

Ufadhili endelevu unahitajika kutopoteza mafanikio yaliyofikiwa katika vita dhidi ya VVU-Msichana Moraa

Afya

"Nimeishi na Virusi Vya Ukimwi tangu mwaka 1992 nilipozaliwa na nimeishi na virusi hivyo maisha yangu yote." Hiyo ni kauli ya Doreen Moraa Moracha, msichana kutoka Kenya ambaye anaishi na VVU kwa miaka 28 sasa.

Doreen Moraa amesema wakati huu dunia ikikabiliwa na janga la virusi vya corona au COVID-19 na watu wengi wenye VVU wakiathirika  yeye amekuwa na bahati kwani."Uwepo wa COVID-19 haujaniathiri sana binafsi kwa sababu nimekuwa na dawa, nilipewa dawa za kipindi cha miezi sita.Tunafanyia kazi  nyumbani kwa hiyo kuonana na watu imekuwa changamoto lakini nimeshuhudia watu wanaoishi na VVU ambao wameathirika sana. Unapata kwamba watu wengi wamepoteza ajira, biashara zimesambaratika na watu walishindwa hata kwenda hospitalini kwa kukosa pesa za kusafiri hadi hospitalini. Unapata pia watu wanalala njaa kwani katika miezi ya awali usambazaji wa chakula haukuwa umeanza na pia kulikosekana septrin ambapo iliwaweka watu wengi wanoishi na VVU katika hali mbaya na wasiwasi huku wakiniuliza kama wanaweza kunywa dawa bila ya septrin."

Katika kuhakikisha kwamba jamii ya kimataifa inaziba ufa ili wasijenge ukuta katika vita dhidi ya VVU Moreen amesema suluhisho ni,"Kuweka ufadhili endelevu ambapo pesa wanazozitoa kwa nchi mbali mbali kutoa msaada kwa waathirika wa VVU ziwe endelevu ili wakati kama huu wa COVID-19 watu hao hawaathiriki kwa kiasi kikubwa kwa kiasi cha hatua ambazo zilikuwa zimekwisha patikana katika kundi la watu wanoishi na VVU zimerudi nyuma kwa sababu maambukizi yanaongezeka idadi ya watu ambao hawakunywi dawa inaongezeka. Pili tusisahau kwamba ijapokuwa tuna COVID-19 tunayokabiliana nayo sasa, tusisahau kwamba HIV imekuwa nasi kwa takriban miaka arobaini, tusisahu kuizungumzia na kuishughulikia tusiacha majadiliano kuihusu ili tusisahau kwamba watu wanoishi na VVU ni waathirika katika ujio huu wa COVID-19."