Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lazima tujitose kwa kila njia kutokomeza hewa ukaa ifikapo 2050: Guterres

Nishati kutokana na upepo.Mwanamke akiendesha baiskeli barabara ya Heijningen, Netherlands.
Unsplash/Les Corpographes
Nishati kutokana na upepo.Mwanamke akiendesha baiskeli barabara ya Heijningen, Netherlands.

Lazima tujitose kwa kila njia kutokomeza hewa ukaa ifikapo 2050: Guterres

Tabianchi na mazingira

Wakati nchi zikihaha kulishinda janga la corona au COVID-19 , pia zina fursa ya kufanikisha azma ya kufanikisha vita dhidi ya mabadiliko ya tabianchi, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amewaambia viongozi wenye ushawishi waliokutana kwa njia ya mtandao leo Jumatatu. 

Antonio Guterres alikuwa akihutubia kongamano la tatu la kila mwaka la Bloomberg New Economy ambalo ni la kimataifa linalowaleta Pamoja serikali, sekta za biashara, teknolojia na wanazuoni. 

Katibu Mkuu amesema “Mwaka 2021 lazima uwe mwaka wa matumaini mapya ya kuelekea azima ya kutokuwa na hewa ukaa. Kila nchi, kila mji, taasisi za kifedha na makampuni yanapaswa kuchukua mipango ya kuhamia kwenye njia ya kutozalisha kabia hewa ukaa ifikapo mwaka 2050.” 

Ishara iliyo bayana 

Bwana. Guterres ameripoti kwamba hivi karibuni Muungano wa Ulaya, Japan, Jamhuri ya Korea Pamoja na nchi nyingine zaidi ya 10 wametangaza ahadi zao za kufikia lengo la kutozalisha kabisa hewa ukaa ambapi Uchina pia inalenga kulifikia mwaka 2060. 

“Mapema mwaka 2021 nchini zinazowakilisha zaidi ya asilimia 65 ya utoaji wa hewa ukaa duniani na zaidi ya asilimia 70 ya uchumi wa dunia zinauwezekano mkubwa wa kutoa ahadi za kutozalisha hewa ukaa.” 

Guterres ameongeza kuwa “Ujumbe unaotumwa na hili kwa masoko, wawekezaji wa taasisi na wafanyamaamuzi ni bayana.Hewa ukaa lazima iwe na gharama. Muda wa kutoa ruzuku kwa mafuta kiskuku umekwisha. Ni lazima kuachane na makaa yam awe, tuanapaswa kuhamishia mzigo wa kodi kutoka kwenye pato na kuelekeza kwenye hewa ukaa, kutoka kwa walipa kodi na kupelekwa kwa wachafuzi.” 

Amesisitiza kwamba utoaji wa taarifa za fedha unaotokana na hatari za mabadiliko ya tabianchi unapaswa kuwa wa lazima, huku mamlaka zikipaswa kujumuisha lengo la kutokomeza hewa ukaa katika sera zake za uchumi na maendeleo ili kuweza kubadili sekta za viwanda, kilimo, usafiri na nishati. 

Katika viunga vya mji mkuu wa Mauritania, Nouakchott, bustani ya mapangaboi ya kuzalisha umeme kwa njia ya upepo  yanaonekana kwa mbali na ni jawabu sahihi katika kuwa na nishati rejelezi
UNDP Mauritania/Freya Morales
Katika viunga vya mji mkuu wa Mauritania, Nouakchott, bustani ya mapangaboi ya kuzalisha umeme kwa njia ya upepo yanaonekana kwa mbali na ni jawabu sahihi katika kuwa na nishati rejelezi

Tuziunge mkono nchi zinazoendelea 

Katibu Mkuu pia amemulika thamani ya ushirikiano baina ya Umoja wa Mataifa na sekta binafsi na za biashara ikiwemo kupitia mkakati kama vile muungano wa wawakezaji wa kimataifa kwa ajili ya malengo ya maendeleo endelevu na muungano kwa ajili ya umiliki wa thamani zisizochafua mazingira. 

Hata hivyo amesisitiza kwamba miungano kama hiyo haiwezi kuwa ya kimataifa bila nchi zinazoendfelea ambazo zinahitaji msaada mkubwa. 

Wakati janga la COVID-19 likiendelea Guterres pia amegusia juhudi zinazoendelea za Umoja wa Mataifa katika kuokoa Maisha, kudhibiti virusi na kupunguza athari. 

Zaidi ya hapo amesema Umoja wa Mataifa unachagiza kile alichokiita “fungu la kujikwamua” kwa nchi na watu wasiojiweza mbali ya kushinikiza hatua za usitishaji uhasama kote duniani. 

“sote tunahaha kukabiliana na janga la corona. Lakini wakati tukifanya hivyo kukomesha mgogoro mmoja pia tuna fursa ya kusshughulikia mwingine.Janga hili limetuonyesha kwamba tunaweza kuwa na upeo mpana Zaidi wa mawazo na kuchukua hatua kubwa wakati wa dharura. Tuna maamuzi muhimu ya kufanya katika wiki na miezi ijayo, hebu tufanye maamuzi ya busara” Amesema Katibu Mkuu.