Lazima tuwaenzi waathirika wa silaha za kemikali:Guterres 

30 Novemba 2020

Katib u Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo amerejea kusisitiza dhamira ya kutokomeza silaha za kemikali duniani huku akitoa wito wa kuwaenzi waathirika wote wa silaha hizo. 

Kupitia ujumbe wake wa maadhimisho ya siku ya kuwakumbuka waathirika wote wa vita vya silaha za kemikali amesema “Matumizi ya silaha hizo popote na kwa yeyote , katika mazingiura yoyote yale ni suala lizilovumilika na ukiukwaji mkub waw a sheria za kimataifa”. 

Katibu Mkuu ameongeza kwamba “Hakuna sababu yoyote inayoweza kuhalalisha matumizi ya silaha hizo za maangamizi. Ni lazima tuendelee kuungana na kudhamiria kuzuia matumizi yake au tishio la matumizi yake , hatuwezi kuruhusu kuwa na kasumba ya kulivumilia hili.” 

Bwana. Guterres pia amekumbusha kwamba ukwepaji sheria kwa matumizi ya silaha za kemikali ni suala lisilokubalika

“Ni muhimu kwa wa;e wanaotumia au waliotumia silaha za kemikali kubainiwa na kuwajibishwa . Hiyo ndiyo njia pekee ya kutekeleza wajibu wetu kimaadili kwa waathirika wa vita vya silaha hizo.” 

Tathimini ya hatua zilizopigwa  

Ujumbe wake pia umesemasiku hii ya kumbukumbu ni fursa ya kuwaenzi waathirika wa ukatili na vitendo hivyo visivyo vya kibinadamu, kutathimini hatua zilizopigwa katika kuzuia matumizi yeyoye ya siku zijazo na kurejea dhamira ya kuzitokomeza silaha hizo duniani kote. Leo hebu turejee ahadi yetu ya kutimiza mkataba kuhusu silaha za kemikali na kutoa msaada wetu kwa shirika la kupinga silaha za kemikali OPCW. Hebu tuwaenzi waathirika wa vita vya silaha hizi kwa kuahidi kuzika silaha hizi katika kurasa za vitabu vya historia.” 

Siku ya kumbukumbu 

Siku hii ya kuwakumbuka waathirika wote wa silaha za kemikali huadhimishwa kila mwaka tarehe 30 Novemba au siku ya kwanza ya kikao cha kawaida cha wadau wa mkutano wa mkataba kuhusu mkataba wa silaha hizo. 

Mbali ya kuwaenzi waathirika siku hii pia inazitaka nchi kuachana kabisa na uwezekano wowote wa matumizi ya silaha hizo kwa kupia utekelezaji wa mkataba wa kupinga silaha za kemikali. 

Kwa mujibu wa OPCW  chombo kinachohusika na utekelezaji wa mkataba huo , zaidi ya asilimia 98 ya akiba ya silaha zote ziliwekwa bayan ana nchi zimeharibiwa chini ya uthibitisho wa OPCW. 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter