Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msipowapatia chanjo watoto wenu dhidi ya Polio watakuwa kama mimi- Richard 

Richard Elaka aliugua Polio akiwa na umri wa miaka 7, na sasa anatumia hali yake kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kupatia chanjo watoto wao wasiugue polio.
UNICEF VIDEO
Richard Elaka aliugua Polio akiwa na umri wa miaka 7, na sasa anatumia hali yake kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kupatia chanjo watoto wao wasiugue polio.

Msipowapatia chanjo watoto wenu dhidi ya Polio watakuwa kama mimi- Richard 

Afya

Kutana na Richard Elaka mkazi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye ni manusura wa ugonjwa wa polio. Yeye anatumia hali yake ulemavu kutokana na Polio kuelimisha jamii umuhimu wa kupatia watoto wao chanjo dhidi ya ugonjwa huo usio na tiba lakini una kinga.

Nyakati za asubuhi, Richard akitembea kwa msaada wa magongo kutokana na ulemavu aliopata baada ya kuugua polio, anaondoka nyumbani tayari kuanza jukumu lake. 
Kwa miaka 24 amekuwa mfanyakazi wa kijamii akitumia simulizi yake ya kuugua polio ili kuelimisha jamii umuhimuwa chanjo dhidi ya polio. 
Nats.. 
Richard anasema asubuhi huamka na kubeba nyaraka zake za kuelimisha jamii kuhusu polio na kuanza kutembelea familia zenye watoto wenye umri kuanzia miezi 0 hadi miezi mitano.” 
Pindi anapofika kwenye familia, huelimisha familia kuwa chanjo ni kitendo cha kuonesha upendo kwa mtoto na kwamba watoto wanao wanapopatiwa chanjo, wanakuwa wamewapatia kinga. Kwa wale wanaopinga je? 
Nats… 
Richard anasema kwa wazazi wanaokataa watoto wao wasipatiwe chanjo, nawaelezea kuwa mimi mwenyewe ni manusura wa Polio. Nitizameni! Iwapo hamtopatia chanjo watoto wenu mtaona madhara yake. Mtoto akipata polio, atakuwa na ulemavu maisha yake yote. Watoto wenu lazima muwapatie chanjo!. 
Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO, linasema polio ni ugonjwa hatari unaoambukika ambao hauna tiba lakini una kinga salama na thabiti  ambayo ni chanjo. 
Chanjo ya polio ikitolewa kwa dozi kadhaa inampatia mtoto kinga maisha yake yote. 
WHO inasema mkakati wa kuzuia polio umejikita katika kuepusha maambukizi miongoni mwa watoto kwa kuwapatia chanjo na kwamba kila mtoto apatiwe chanjo hadi dunia nzima itakapokuwa haina hata kisa kimoja cha polio. 
Hadi sasa ni nchi tatu tu zenye polio ambazo ni Nigeria, Pakistan na Afghanistan.