Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hewa ya ukaa, CO2 angani imebaki katika viwango vya juu licha ya janga la COVID-19: WMO 

Viwango vya hewa ukaa vinaendelea katika kiwango cha rekodi ya juu, licha ya kushuka kwa uchumi kusababishwa na janga la COVID-19.
Unsplash/Johannes Plenio
Viwango vya hewa ukaa vinaendelea katika kiwango cha rekodi ya juu, licha ya kushuka kwa uchumi kusababishwa na janga la COVID-19.

Hewa ya ukaa, CO2 angani imebaki katika viwango vya juu licha ya janga la COVID-19: WMO 

Tabianchi na mazingira

Wataalam wa WMO wameeleza kuwa licha ya kupungua kwa uzalishaji wa viwandani kwa sababu ya janga la COVID-19 na karantini, mkusanyiko wa hewa ya ukaa, CO2 angani bado uko juu. 

Tathimini ya WMO imeeleza kuwa mnamo mwaka 2020, uzalishaji wa hewa chafuzi ulipungua, lakini mabadiliko katika mkusanyiko wa hewa ya ukaa CO2 hayakuwa sawa na ikilinganishwa na wastani wa viwango vya kushuka kila mwaka.  

Kwa mujibu wa makadirio ya awali, kiwango cha kimataifa cha uzalishaji hewa chafuzi kitapungua katika mwaka huu wa 2020 kwa angalau asilimia 4.2, na kwa kiwango cha juu asilimia 7.5. Kama wataalam wanavyosisitiza, hii haitasababisha kupungua kwa kiwango cha mkusanyiko wa hewa ya ukaa yaani CO2 angani. 

Vile vile kwa mujibu wa wataalam, tangu mwaka 1990 jumla ya mionzi ya kuzalisha hewa chafuzi kulazimisha imeongezeka kwa asilimia 45. 

Tweet URL

Katibu Mkuu wa WMO Petteri Taalas amesema, “Hewa ya ukaa inabaki katika anaga kwa karne kadhaa na inasalia kwa muda zaidi katika bahari. Mara ya mwisho kulinganishwa kwa mkusanyiko wa hewa ya ukaa duniani kuliangaliwa miaka milioni 3 hadi 5 iliyopita wakati ambapo viwango vya joto vilikuwa nyuzi 2 hadi 3  juu zaidi  na kina cha bahari kilikuwa mita 10 hadi 20 juu kuliko hivi sasa. Lakini sayari haikuwa na watu bilioni 7.7.” 

Bwana Taalas anasisitiza kuwa haiwezekani kuchukulia janga kama suluhisho la shida ya ongezeko la joto duniani. Wakati huo huo, kulingana na kiongozi huyo wa WMO, janga na mabadiliko ambayo yametokea ndani ya mfumo wa janga lenyewe yanaweza kuwa mahali pa kuanzia kwa hatua zaidi za kupunguza uzalishaji hewa chafuzi unaodhuru na kupambana na ongezeko la joto duniani. 

Bwana Taalas amehitimisha akisema, "hatua zinazohitajika zinapatikana kiuchumi na kitaalam zinawezekana, na zitaathiri kwa kiasi maisha yetu ya kila siku. Tunakaribisha ukweli kwamba idadi kubwa ya nchi na makampuni wanachagua kutokuwepo kwa hewa ya ukaa.kaboni.”