Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Unaweza kuwa chochote utakacho la msingi imani na kujitume:Mohammed 

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Amina Mohammed akiwa na mpira wa soka uliochorwa SDGs akiwa mji mkuu Abuja nchini Nigeria.
United Nations/Daniel Getachew
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Amina Mohammed akiwa na mpira wa soka uliochorwa SDGs akiwa mji mkuu Abuja nchini Nigeria.

Unaweza kuwa chochote utakacho la msingi imani na kujitume:Mohammed 

Utamaduni na Elimu

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Amina J. Mohammed ambaye yuko ziarani Afrika Magharibi na ukanda wa Sahel amewachagiza wasichana katika eneo la Maiduguri jimbo la Borno nchini Nigeria kufanya kila wawezalo kutimiza ndoto zao kwani hakuna linaloshindikana. 

Naibu Katibu Mkuu Bi. Amina Mohhamed aliwasili  jimboni Borno akitokea Abuja na kisha kupanda helkopta hadi mjini Banki eneo la Bama karibu na mpaka na Cameroon  ambako alikutana na viongozi mbalimbali na kuwatembelea wakimbizi wa ndani pamoja na wakimbizi wa Nigeria wanaorejea kutoka Cameroon. 

Huko pia alikagua jengo la Umoja wa Mataifa, ukuta na kituo cha ukaguzi cha mpakani kabla ya kukelekea Maiduguri ambako alibahatika kuzungumza na wanafunzi wa shule ya wasichana ya Gomari Mega na kuwachagiza licha ya changamoto wanazopitia kutokata tamaa ya kutimiza ndoto zao “Watu wanaponiona Umoja wa Mataifa ninawakumbusha kwamba nilianzia shule hapa Maiduguri. Hivyo unaweza kuwa mtu yeyote unayetaka, unachotakiwa ni kujituma, kuamini na kufanya yaliyo sahihi na lazima uwe na Imani. Iwe imani yoyote ile ilimradi uwe nayo. Leo ninavyowaona nyie nyote nahamasika kwa sababu naamini mustakabali wa Nigeria ni mzuri  na wa matumaini kwa Nigeria.”

Jimbo la Borno limeghubikwa na changamoto nyingi kuanzia vita, wakimbizi na tatizo kuwa la uasi wa Boko Haram kundi la kigaidi ambalo tarehe 14 Aprili 2014 lilivamia shule ya wasichana Chibok na kuwateka wanafunzi 2019. 

Na baada ya kuaga Maiduguri jimboni Borno Bi. Mohammed ameelekea Niger.