Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres ashtushwa na vifo vilivyosababishwa na kimbunga Eta Amerika ya Kati

Pia za NASA zikionyesha kimbunga Eta kikiwasili Amerika ya Kati
NAMS
Pia za NASA zikionyesha kimbunga Eta kikiwasili Amerika ya Kati

Guterres ashtushwa na vifo vilivyosababishwa na kimbunga Eta Amerika ya Kati

Msaada wa Kibinadamu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ameshtushwa na kusikitishwa na vifo vilivyotolea leo Jumamosi kwa sababu ya kimbunga Eta kinachokumba Amerika ya Kati.

Kimbunga hicho kilichotajwa kuwa katika daraja la nne kimesababisha pia uharibifu mkubwa , na kilikumbwa pwani ya Nicaragua siku ya Jumannekabla ya taratibu kuelekea nchini Honduras.

Kimbunga hicho kimesababisha mvua kubwa katyika eneo lote la Amerika ya Kati ambayo imesabisha mafuriko na maporomoko ya udongo hususan nchini Guatemala.

“Janga hili la asili linatokea wakati ukanda huo mzima unahaha kukabiliana na janga la corona au COVID-19imesema taarifa hiyo ya Katibu Mkuu iliyotolewa leo na msemaji wake Stephane Dujarric.

Katibu Mkuu ameyuma salamu za rambirambi kwa familia za waathirika na kwa wat una serikali za ukanda huo. Pia amewatakia majeruhi wote ahuweni ya haraka.

Guterres amepongeza juhudi za wote ambao wanafanya kila liwezekanalo kufikisha misaada kwa watu wa ukanda huo.Taarifa imeongeza kwamba Guterres

“Ameonyesha mshikamano na serikali na watu wa ukanda huo na kusisitiza kwamba Umoja wa Mataifa uko tayari kushirikiana nao kukidhi mahitaji ya kibinadamu yaliyosababishwa na athari za kimbunga hicho.”