COVID-19 imeongeza visa vya ukatili wa kijinsia Kenya:Healthcare Assistance

6 Novemba 2020

Shirika lisilo la kiserikali la Heathcare Assistance Kenya, limesema janga la corona au CIVID-19 limezidisha visa vya ukatili wa kijinsia ambapo kati ya Machi hadi Oktoba mwaka huu visa zaidi ya 5000 vya ukatili wa kijinsia vimeripotiwa katika shirika hilo.

Shirika la Healthcare Assistance ambalo linasaidiwa kwa kiasi fulani na shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu duniani UNFPA limelivalia njuga suala ya ukatili wa kijinsia nchini Kenya (GBV) ambalo duniani kote kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa linamuathiri mwanamke 1 kati ya 3 katika maisha yake. 

Na ukatili huu unajumuisha pia ukeketaji ambapo takwimu za UNFPA zinaonyesha kwamba umewaathiri wanawake na wasichana milioni 200 kote duniani.
Miongoni mwa hatua zilizochukuliwa na Healthcare Assitance nchini Kenya ni pamoja na kuanzisha huduma ya namba maalum ya simu 1195 ambapo watu hupiga bure na kuripoti matukio ya ukatili wa kijinsia. Fanis Lisiagali ni mkurugenzi mkuu wa shirika hilo anafafanua huduma hii inafanyaje kazi? 

Ameongeza kuwa janga linaloendelea la COVID-19 limekuwa msumari wa moto juu ya kidonda  katika masuala ya ukatili wa kijinsia

Bi. Lisiagali anasema ingawa wanaopiga simu kupata msaada ni wa jinsia zote lakini asilimia kubwa ni wanawake na wasichana. 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter