Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwanasheria Paul Gicheru wa Kenya awasili kizuizini ICC 

Makao makuu ya mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai, ICC huko The Hague, Uholanzi
UN /Rick Bajornas
Makao makuu ya mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai, ICC huko The Hague, Uholanzi

Mwanasheria Paul Gicheru wa Kenya awasili kizuizini ICC 

Sheria na Kuzuia Uhalifu

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC imesema jana Jumanne Novemba 3 mamlaka ya Uholanzi ilimkabidhi Paul Gicheru kwenye mahakama hiyo. 

Bwana Gicheru mwanasheria wa zamani wa Kenya anashukiwa kwa makosa dhidi ya usimamizi wa haki yakiwemo ya kuwashawishi vibaya mashahidi wa mahakama. 

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya ICC Bwana Gicheru alijisalimisha kwa mamlaka ya Uholanzi tarehe 2 Novemba 2020 kufuatia kibali cha kukmatwa kilichotolewa na mahakama hiyo mwaka 2015. 

Kisha mamlaka ya Uholanzi jana ikimsafirisha na kumkabidhi mikononi mwa ICC baada ya kukamilisha mipango ya kitaifa ya kumkamata na sasa yuko kiuzuizini kwenye kituo cha mahakama hiyo. 

Hatua inayofuata 

ICC inasema hatuia inayofuata ambayo itakuwa siku si nyingi ni kwa mshukiwa huyo kupanda kizimbani kwa mara ya kwanza katika mahakama hiyo.  

Na katika tukio hilo kitengo cha mahakama kitathibitisha uraia wa mshukiwa na kuhakikisha kwamba mshukiwa anaelewa makosa, kuthibitisha lugha ambayo itatumika kuendesha mashitaka na kupanga tarehe ya kuanza kusikiliza kesi ya kuthibitisha mashitaka yake. 

Kibali cha kukamatwa kwa Bwana. Gicheru na Philp Kipkoech Bett kilitolewa na mahakama ya ICC mnamo 10 Machi 2015. Bwana Philp Kipkoech bado hajakamatwa na hayuko mikonini mwa ICC.