Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yaongeza nguvu kuzuia kusambaa kwa COVID-19 kambini Cox’s Bazar 

Mhudumu wa afya akitoa huduma Cox's Bazar nchini Bngladesh.
IOM/Nate Webb
Mhudumu wa afya akitoa huduma Cox's Bazar nchini Bngladesh.

WHO yaongeza nguvu kuzuia kusambaa kwa COVID-19 kambini Cox’s Bazar 

Afya

Ili kusaidia kusambaa kwa COVID-19 miongoni mwa wakimbizi wa Rohingya katika kambi ya Cox's Bazar, nchini Bangladesh, Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa, WHO na washirika wake wanaongeza ufuatiliaji na upimaji wa magonjwa, kuanzisha vituo vya matibabu na kuihusisha jamii ili wakazi wa kambi wajue kujilinda na familia zao.

 

Mitaani Cox’s Bazar, kambi ya kambi ya wakimbizi wa Rohingya nchini Bangladesh, msongamano wa watu na nyumba ni wa wazi. 

(Nats)

Shughuli zinaendelea. Wa kuuza wanauza, wa kununua wananunua, ilimradi ni pilika za hapa na pale. 

WHO na wadau wake wamefanya kazi kwa bidii kusaidia kuzuia kusambaa kwa COVID-19 kati ya wakimbizi wa Rohingya walio katika mazingira magumu katika kambi  hii.  Ufuatiliaji wa magonjwa, upimaji na ufuatiliaji wa watu waliokutana na walioambukizwa au wanaohisiwa kuambukizwa, umeimarishwa. 

Dkt Khadimul Alam Mazhar, Mshauri kuhusu uchunguzi wa milipuko ya magonjwa wa WHO anapita kambini kufuatilia wanaoweza kuwa wameambukizwa na anazungumza na mkimbizi Mahmuda Begum kisha anajaza takwimu katika Apu ya Go.Data iliyoko kwenye simu ya kiganjani. Dkt Mazhar anasema,  "Kwa kweli ni ngumu kutekeleza hatua kadhaa za kiafya za umma ambazo zimependekezwa ulimwenguni dhidi ya janga hili. Kama unavyojua, katika kambi, wakimbizi wanaishi katika hali ya watu wengi, lakini WHO na washirika wa sekta ya afya, wanafanya kazi kila wakati kuhakikisha kwamba hatua hizi za afya ya umma zinatekelezwa kupitia mawasiliano na ushiriki wa jamii. Pia tuna wahudumu wa afya waliojitolea ambao wanatembelea nyumba kwa nyumba kutoa ujumbe huu kwa jamii.” 

Mkimbizi Mahmuda Begum akiwa ameketi katika mlango wa makazi yake anasema, “Kambi hii ina watu wengi; nyumba hazina mwanya katikati. Hatuwezi kuweka umbali kati ya mt una mtu. Kuna watu wengi wanasukumana. Kuna uhaba wa maji na uhaba wa sabuni, hii inaleta ugumu.”   

WHO inafanya kila juhudi, vifaa vya matibabu vimewekwa, na Taasisi ya maabara ya udhibiti na utafiti wa magonjwa, IEDCR imeimarishwa. 

Kama ilivyo kwa hatua ya mlipuko wowote wa ugonjwa, ushiriki wa jamii pia ni muhimu ili wakazi wa kambi hii ya Warohingya wajue jinsi ya kujilinda na familia zao, kwa hivyo WHO imewashirikisha wana jamii.