Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lazima tushikamane na kusaidiana kwa pamoja tunaweza:Inspekta Malambo 

Inspekta mkuu Doreen Malambo ambaye ni mshauri wa masuala ya kijinsia kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS)
UNMISS
Inspekta mkuu Doreen Malambo ambaye ni mshauri wa masuala ya kijinsia kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS)

Lazima tushikamane na kusaidiana kwa pamoja tunaweza:Inspekta Malambo 

Amani na Usalama

Inspekta mkuu Doreen Malambo raia wa Zambia ambaye ni mshindi wa tuzo ya Umoja wa Mataifa ya afisa wa polisi kwa mwaka wa 2020, leo amekabidhiwa tuzo yake katika hafla maalum iliyofanyika kwa njia ya mtandao.

Mjini Juba Sudan Kusini katika taifa changa kabisa duniani lililoghubikwa na vita vya wenyewe kwa wenye ndiko anakohudumu inspekta mkuu Malambo kama mshauri wa masuala ya jinsia, ambako kwa mara ya kwanza aliwasili mwaka 2016 mchafuko yakiwa yameshika kasi  anasema alishuhudia madhila na machungu ya hali ya juu,“Sikuwa na mwelekeo wowote siku ya kwanza ya machafuko , siku ya pili bila shaka tulikuwa tukifuatilia matangazo ya redio na walipotoa ombi la maafisa wa UNPOL kujitokeza na kusaidia watu wa Sudan Kusini ambao walikuwa wanakimbilia kambini, nilikuwa mwanamke wa kwanza kujitokeza sikuwa hata na vesti ya kujilinda” 

Kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu UNFPA  Inspekta Malambo alianzisha mkakati wa kusimamia haki za wanawake na wasichana ambao umesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza  na kuzuia ukatii wa kingino na uhalifu wa kijinsia Sudan Kusini na kama sehemu ya mkakati huo aliunda mtandao wa makundi yaliyoongozwa na maafisa wa polisi wanaume ili kuhusisha wanaume katika jamii kusambaza taarifa na kuchagiza ulinzi na usongeshaji wa haki za wanawake na wasichana. “Nilipomaliza muda wangu Sudan Kusini mwaka 2018 nilikaa nchini mwangu miezi mitatu tu na nikaitwa tena haraka kurejea kwasababu ya kazi yangu iliyotambuliwa ya kuwawezesha wanawake.” 

Inspekta Malambo anasema anaamini kwa kushikamana na kusaidiana hakuna linaloshindikana.Tuzo ya Umoja wa Mataifa ya afisa wa polisi wa mwaka mwanamke ilianzishwa mwaka 2011 kutambua mchango mkubwa wa wanawake maafisa wa polisi katika operesheni za amani za Umoja wa Mataifa na kuchagiza uwezeshaji wa wanawake.   

Na mwaka huu tuzo hiyo ina umuhimu mkubwa zaidi kwani azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa namba 1325 kuhusu wanawake, amani na ulinzi linaadhimisha miaka 20, lakini pia ni miaka 60 tangu polisi wa kwanza wa UNPOL walipopelekwa kwenye operesheni za amani za Umoja wa Mataifa nchini Congo. 

Na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake kwenye hafla hiyo amesema “Leo hii kuna polisi 11,000 wa UNPOL na 1,300 kati yao ni wanawake ambao wanahudumu katika operesheni 16 za amani ili kuimarisha amani na usalama wa kimataifa kwa kusisaidia nchi katika mizozo, baada ya mizozo na katika migogoro mingine.” 

Lengo la Umoja wa Mataifa ni kupeleka asilimia 30 ya wanawake miongoni mwao maafisa wa polisi na asilimia 20 ya kitengo cha polisi ifikapo mwaka 2028.