Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wazazi wa kiume Ethiopia waitikia wito wa kukabili Surua  

Mtoto akipatiwa chanjo dhidi ya surua wakati wa kampeni ya chanjo huko Impfondo, Jamhuri ya Congo
© UNICEF/Mariame Diefaga
Mtoto akipatiwa chanjo dhidi ya surua wakati wa kampeni ya chanjo huko Impfondo, Jamhuri ya Congo

Wazazi wa kiume Ethiopia waitikia wito wa kukabili Surua  

Afya

Ethiopia, kampeni ya kitaifa ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa surua iliyoanza mwezi Juni mwaka huu, imeanza kuonesha mwitikio mkubwa hata miongoni mwa wazazi wa kiume.

 

Kutana na Daniel, anatoka Ethiopia, akiwa ameketi anasema mwanangu wa kike aliugua! Alipumua kwa taabu sana na kutoa pumzi nzito kama mtu mzima! 

Baba huyu anasema kuwa ugonjwa huo ambao hata hawakutambua ulimsababishia mwanae huyo wa kike maumivu makali kiasi kwamba alilazimika kuacha kazi kwa sababu hakuweza kumakinika. 

Daniel anasema alipoteza kabisa hamu ya kula na akajawa na hofu kila wakati. 

Katika eneo lao, mhudumu wa afya Mekdes Tesfaye pamoja na wenzake walipata taarifa kuhusu watoto kuugua na hata wengine kufariki dunia, na ndipo walipoanza ziara za nyumba kwa nyumba. “Tuliwaelimisha kuwa siyo ugonjwa wa Corona au COVID-19 bali ni Surua. Tunawaelimisha kuhusu utapiamlo, kwa hiyo wale lishe bora. Na sasa tunaona mabadiliko makubwa. Kituo cha afya kinatoa huduma bado kwa mama na mtoto.” 

Ziara za Mekdes zilimfungua macho Daniel akisema,  Anasema mhudumu wa afya alipomuona tu, alisisitiza lazima tumpeleke haraka kituo cha afya. Niliamua kumpeleka mwanangu haraka nikisema afe au apone, chochote kile kitokee akiwa kituo cha afya. Alilazwa kituoni kwa siku 10. Hali yake taratibu iliimarika na kisha akapona, nilifurahi sana.” 

Daniel anakiri kuwa iwapo asingalimpeleka mwanae kituo cha afya, angalifariki dunia. 

Sasa mawazo na hofu kuhusu mwanae vimeondoka na tabasamu na vicheko vimeshamiri kwenye familia yake yeye, mkewe na mwanae.