Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN yaipongeza Jamhuri ya korea kwa ahadi ya kukomesha uzalishaji wa hewa ukaa 

Miji kama mji mkuu wa Korea Kusini Seoul ni watumiaji wakubwa wa nishati
Unsplash/Ethan Brooke
Miji kama mji mkuu wa Korea Kusini Seoul ni watumiaji wakubwa wa nishati

UN yaipongeza Jamhuri ya korea kwa ahadi ya kukomesha uzalishaji wa hewa ukaa 

Tabianchi na mazingira

Ahadi ya Jamhuri ya Korea ya kufanikisha kutokuwepo kwa hewa ukaa ifikapo mwaka 2050 imepongezwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kama “Ni hatua nzuri sana katika mwelekeo sahihi” 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wake, mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ametiwa moyo sana na tangazo lililotolewa leo na Rais Moon Jae-In wa Korea Kusini wa kufikia kutozalisha hewa ukaa ifikapo mwaka huo 

Kundi linazidi kuongezeka 

Kwa tangazo hili Jamhuri ya Korea inayoshika nafasi ya 11 kwa uchumi mkubwa duniani na nafasi ya sita kwa usafirishaji bidhaa nje inajiunga na kundi linaloongezeka laenye uchumi mkubwa uliojitolea kuwa msitari wa mbele na kuongoza kwa mfano katika kujenga ulimwengu endelevu , usio na hewa ukaa na ulimwengu wenye mnepo dhidi ya amabdiliko ya tabianchi mwaka 2050 imeongeza taarifa hiyo. 

Rais Moon aliweka nadhiri katika hotuba yake kwa bunge la kitaifa ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi sanjari na tangazo la dola bilioni 35 zilizotangazwa mwezi Julai la kusaidia masuala ya mazingira na kukomesha uwekezaji katika makaa ya mawe. 

Katibu Mkuu ameelezea hatua hiyo kama “Ni hatua nzuri katika mwlekeo sahihi baada ya mpango mpya wa Jamhuri ya Korea wa kulinda mazingira.” 

Tangazo hilo limekuja siku mbili tu baada ya Japan kusema itafikia kkiwango cha kutokuwa na hewa ukaa ifikapo mwaka 2050, tangazo ambalo pia limekaribishwa na Bwana. Guterres. 

Malengo makubwa zaidi 

Katibu MKuu kwa muda mrefu amekuwa akipigia chepuo hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kuwa ni kipaumbele cha uongozi wake. 

Akizungumza na mawaziri wa fedha wa kimataifa mapemamwezi huu alitoa wito kwa nchi kuongeza juhudi zao na kujitolea ili kufikia lengo la kutokuwa na hewa ukaa hasa katika suala la uzalishaji wa gesi chafuzi. 

Pia alizihimiza nchi kuwasilisha michango yao yenye dhamira zaidi ya kitaifa (NDCs) ikielezea hatua ya kupunguz uzalishaji na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kama inavyotakiwa chini ya mkataba wa Paris wa 2015 kuhusu mabadiliko ya tabaianchi. 

Sasa Katibu Mkuu anatarajia hatua madhubuti za sera ambazo zitapendekezwa na kutekelezwa na Korea Kusini, imesema taarifa hiyo. 

Hii ni Pamoja na kuwasilisha NDC iliyorekebishwa ambayo inakwenda sanjari na dhamira yake mpya.