Viwango vya unyafuzi Yemen vyavunja rekodi- UNICEF
Viwango vya unyafuzi Yemen vyavunja rekodi- UNICEF
Unyafuzi au utapiamlo uliokithiri umeshika kasi miongoni mwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 nchini Yemen ambapo takwimu mpya zinaonesha kuwa zaidi ya watoto 500,000 kwenye wilaya 13 kusini mwa nchi hiyo wana unyafuzi.
Mjini Aden, nchini Yemen, kukurukakara zikiendelea, sambamba na katika kituo cha afya, watoto wakifika kupatiwa tiba dhidi ya unyafuzi.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na wadau wake wametoa takwimu zinazoonesha ongezeko la asilimia 10 la watoto wenye unyafuzi mwaka huu pekee na kati yao hao 98,000 wako hatarini kufariki dunia iwapo hawapati fedha za kuwapatia misaada kama vile lishe bora na huduma za afya.
Miongoni mwa watoto hao ni Afnan Fein akiwa amefika kituo cha afya cha na mama yake mzazi, Mariam Salem Ahmed ambapo anapimwa unyafuzi na kisha kupatiwa kipaketi chenye mchanganyiko wa lishe bora. Ashjan Abdullah Ahmed ni mhudumu wa afya. “Natumai msaada huu wa lishe utaendele kwa sababu kuna wagonjwa ambao wanapata ahueni, tunashukuru sana mwanao kwa sasa hana tena utapiamlo. Na hawa wanatueleza kuwa nyumbani hawana tena chakula. Wana chakula hiki cha msaada. Hata mchanganyiko wa soya tunaopatia wajawazito na wanawake wanaonyonyesha wanasema umekwisha. Watu wanafurahia sana chakula hiki.”
Mtoto mwingine Rafiq Bassam Ali Hassan naye anapimwa utapiamlo na kisha mama yake Intisar Abdullah Ibrahim anafunguka,
“Hali ilikuwa ngumu sana na janga hili la coronavirus">COVID-19. Hatukuweza tena kujikimu mahitaji yetu ya kila siku. Tulihofia sana kutoka nje.”
Yemen inaslia kuwa nchi inayoongoza duniani kwa janga la kibinadamu ambapo takribani raia milioni 24, saw ana asilimia 80 ya wananchi wake wanahitaji msaada wa kibinadamu na ulinzi.