Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chonde chonde Tanzania fanyeni uchaguzi kwa amani:OHCHR

Wananchi katika moja ya mitaa ya jiji la Dar es salaam, Tanzania. Picha ya MAKTABA
UN-Habitat/Julius Mwelu
Wananchi katika moja ya mitaa ya jiji la Dar es salaam, Tanzania. Picha ya MAKTABA

Chonde chonde Tanzania fanyeni uchaguzi kwa amani:OHCHR

Haki za binadamu

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR, leo imetoa wito kwa wadau wote nchi Tanzania kuhakikisha uchaguzi mkuu unaofanyika kesho Jumatano Oktoba 28, unakuwa wa amani, jumuishi na shirikishi, kwa watu kuweza kupiga kura zao kwa uhuru bila hofu na vitisho. 

Akizungumza na waandishi wa Habari kwa njia ya mtandao mjini Geneva Uswis hii leo msemaji wa ofisi hiyo ya haki za binadamu Ravina Shamdasan amesema “Tumekuwa tukifuatilia kwa hofu kusinyaa kwa demokrasia nchini humo huku kukiwa na ripoti za kusikitisha za vitisho, udhalilishaji, watu kukamatwa na mashambulizi dhidi ya wanasiasa wa upinzani, waandishi wa Habari, wanawake watetezi wa haki za binadamu na wanaharakati wengine.” 

Ameongeza kuwa ukandamizaji huu wa sauti za upinzani umeongezeka wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu, ambapo haki za uhuru wa kujieleza na ushiriki wa kisiasa vinapaswa kuzingatiwa, sio kukandamizwa. Uchaguzi huo mkuu wa Rais na wabunge unafanyika kesho. 

Bi. Shamdasani pia amesema “Tumetiwa hofu haswa na ripoti kwamba watu watatu wamearifiwa kuuawa jana usiku na wengine kujeruhiwa Pemba katika visiwa vya Zanzibar, ambapo polisi walifyatua risasi za moto katika makabiliano na wafuasi wa upinzani.” 

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharib Unguja visiwani Zanzibar Awadhi Juma Haji akizungumzia hali ilivyo amesema 

Kwa mantiki hiyo ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeitaka mamlaka nchini humo kuhakikisha kunafanyika uchunguzi wa haraka, wawazi na huru wa tukio hilo na kutoa wito kwa wadau wote katika uchaguzi kujizuia na vitendo vyovyote vya machafuko.