Mshikamano wa kuanzisha UN miaka 75 iliyopita utumike kutokomeza COVID-19

Wawakilishi kutoka nchi 50 wakiwa kwenye kikao kilichofanyika San Francisco nchini Marekani, kikao kilichofanikisha kuanzishwa kwa Umoja wa mataifa.
UN Photo/Rosenberg
Wawakilishi kutoka nchi 50 wakiwa kwenye kikao kilichofanyika San Francisco nchini Marekani, kikao kilichofanikisha kuanzishwa kwa Umoja wa mataifa.

Mshikamano wa kuanzisha UN miaka 75 iliyopita utumike kutokomeza COVID-19

Masuala ya UM

 Kuelekea siku ya Umoja wa Mataifa kesho ambapo chombo hicho kinatimia miaka 75 tangu kuanzishwa kwake, Anold Kayanda anatupitisha safari ya kuanzishwa chombo hicho na matarajio ya siku za usoni. 

Mwaka 1945 jijini San Francisco nchini Marekani wajumbe kutoka mataifa 50 walikutana kujadili kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa! Ni baada ya vita kuu mbili za dunia kudhihirisha kuwa vita si suluhu ya amani duniani! Baada ya majadiliano ya kina mwenyekiti wa kikao akapaza sauti! Anasema... Na sasa ni wajibu wangu, na kwa heshima kubwa kuitisha upigaji kura ya kupitisha chata ya Umoja wa Mataifa ikiwemo mkataba wa mahakama ya kimataifa, na kwa heshima kubwa hebu na niwakaribishe viongozi wa ujumbe ambao wanaunga mkono kupitishwa kwa chata na mkataba wanyanyuke kwenye viti vyao na wasalie vivyo hivyo wanapohesabiwa!” 

 Na wajumbe waliridhia! Kilichofuatia ni wawakilishi wa nchi 50 mmoja baada ya mwingine kutia saini Chata ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa inayoanza kwa utangulizi Sisi Wakazi wa Dunia tumeazimia.. kisha mwenyekiti akasema.. 

 AnasemaKuna wengi walikuwa na shuku kuwa makubaliano yasingalifikiwa baina ya nchi hizi 50 zenye tofauti kubwa kwa rangi, dini, lugha na utamaduni. Lakini tofauti zote hizi zilisahaulika kupitia umoja usiotikisika wa kusaka mbinu za kumaliza vita.” 

Kadri siku zilivyosonga, na manufaa ya Umoja wa Mataifa kuonekana, mwaka 1960 mataifa ya 14 ya Afrika yanayozungumza lugha ya kifaransa yalijiunga na chombo hicho! Bendera zilipandishwa kwenye jengo la makao makuu ya Umoja wa Mataifa na Katibu Mkuu wakati huo Dag Hammarskjöld akasema,“Tuna mambo mengi ya kufanana kiasi kwamba tushinde kubadili maadili ya kibinadamu ambao ndio urithi wetu wa pamoja unaoweza kuunganisha uthabiti wetu na kuishi kwa pamoja kwa amani.” 

 Miaka 75 tangu kuanzishwa chombo hicho, janga la Corona limetikisa ulimwenguni!  Wakati wa tamasha la muziki la miaka 75 ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza kwenye tukio hilo amesema mshikamano wa kuanzisha Umoja wa Mataifa utumiwe na wanachama 193 kutokomeza COVID-19“Katika siku ya Umoja wa Mataifa, nasisitiza ombi langu la sitisho la mapigano duniani ili sote tuweze kuelekeza nguvu zetu kwenye vita dhidi ya COVID-19. Hebu sote na tushinde janga hili, tuzuie janga la mabadiliko ya tabianchi, kuzingatia usawa wa wanawake na wanaume na kufungua njia kwa dunia salama, yenye afya na endelevu.”