Kila upande katika mgogoro wa Nagorno-Karabakh unapaswa kulinda raia:UN

18 Oktoba 2020

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo amelaani vikali mashambulio yote katika maeneo yaliyo na watu wengi ndani na katika viunga bvya ukanda wa mapigano wa Nagorno-Karabakh, wakati duru zikiripoti kwamba pande zote katika mgogoro huo za Azerbaijan na Armenia zikilaumiana kwa kukiuka makubaliano ya karibuni ya usitishaji uhasama kwa misingi ya kibinadamu.

Kupitia taarifa iliyotolewa na msemaji wake Jumapili ya leo Antonio Guterres ameelezea“zahma ya kupotea kwa Maisha ya raia wakiwemo Watoto kutokana na mshambulizi ya anga yaliyioripotiwa Oktoba 16 kwenye mji wa pili kwa ukubwa nchini Azerbaijan wa Ganja kuwa ni jambo lisilokubalika kabisa.”

Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa pia amesisitiza kwamba“Mashambulizi yayisiyo ya kulenga katika maeneo yenye watu wengi popote ikiwemo Stepanakert/Khankendi na maeneo ya jirani ndanbi ya katika vunga vya ukanda wa mapambano wa Nagorno-Karabakh, pia ni jambo lisilokubalika.”

Pande zote zimeafiki makubaliano ya amani kuanza usiku wa jana Jumamosi kwa saa za eneo hilo kufuatia Urusi na viongozi wengine wa kundi la Minsk kwa ajili ya mkutano wa usalama na ushirikiano barani Ulaya (OSCE) ulioundwa mwaka 1992 kuingilia kati na kuchagiza suluhu ya amani kwa mgogoro wa Nagorno-Karabakh baina ya nchi hizo mbili zilizo kitovu cha mgogoro.

Kundi hilo linaongozwa chini ya uenyekiti wa Marekani, Ufaransa na Urusi na wajumbe wake wa kudumu ambao ni Belarus, Ujerumani, Italia, Sweden, Finland, Uturuki, Armenia na Azerbaijan.

Ni masikitiko kuendelea kwa machafuko

Katibu Mkuu Guterres amesema “Nasikitika sana kwamba pande zote zimeendelea kupuuza wito unaotolewa kila uchao na jumuiya ya kimataifa wa kusitisha mara moja mapigano”.

Pia amesisitiza kwamba “Amehimiza tena katika wito wake wa karibuni kwa mawaziri wa mambo ya nje wa Armenia na Azerbaijan, kwamba pande zote zina wajibu chini ya sheria za kimataifa za kibinadamu kuchukua hatua za kuwalinda rai ana miundombinu yao katika operesheni zao za kivita.”

Mkuu huyo wa Umoja wa Mastaifa amesema anatambua makubaliano mapya ya amani ambayo yamekuja muda mfupi baada ya sjambulio la kombora lililoarifiwa kuua na kujeruhi watu kadhaa Jumamosi mjini Ganja.

Taarifa hiyo imehitimisha kwa kusema “Kastibu Mkuu anatambua tangazo la karibuni la kuanza makubaliano ya amani ya kibinadamuleo 18 Oktoba na kutarajia pande zote kuheshimu makubaliano hayo na kuanza majadiliano ya kina bila kuchelewa chini ya mwamvuli wa viongozi wa kundi la Minski OSCE.”

 

 

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter