Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

COVID-19 kutumbukiza mamilioni zaidi ya watu katika umasikini:Guterres

Katikati ya siku yenye jotot katli mwendesha baisekli akipumzika kando ya barabara Dhaka nchini Bangladesh.
IMF
Katikati ya siku yenye jotot katli mwendesha baisekli akipumzika kando ya barabara Dhaka nchini Bangladesh.

COVID-19 kutumbukiza mamilioni zaidi ya watu katika umasikini:Guterres

Afya

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kutokomeza umasikini, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema janga la corona au COVID-19 litawatumbukiza mamilioni ya watu zaidi katika janga la umasikini. 

Kupitia ujumbe wake maalum kwa siku hii Antonio Guterres amesema COVID-19 ni janga juu ya janga kwa watu masikini duniani kutokana na sababu kuu mbili. 

“Mosi ndio walio katika hatari kubwa ya kupata virusi hivyo na ndio watu wasio na fursa ya huduma bora za afya. Pili makadirio ya hivi karibuni yanaonyesha kwamba janga la COVID-19 linaweza kuwasukumua hadi watu milioni 115 kutumbukia kwenye umasikini mwaka huu, ikiwa ni ongezeko la kwanza la umasikini kwa miongo kandhaa, huku wanawake wakiwa katika hatari kubwa zaidi kwa sababu ndio walio na uwezekano mkubwa wa kupoteza kazi zao na pia kukosa ulinzi wa hifadhi ya jamii.” 

Bwana. Guterres amesisitiza kwamba hizi ni nyakati ngumu ambazo zinahitaji juhudi za hali ya juu kupambana na umasikini na janga la COVID-19 linahitaji juhudi imara za pamoja kulikabili. 

Amehimiza kwamba “Serikali lazima zisongeshe mabadiliko ya kiuchumi kwa kuwekeza kwenye ujikwamuaji endelevu na unaojali mazingira.Tunahitaji kizazi kipya chenye mipango ya ulinzi wa hifadhi ya jamii ambayo itawalinda pia watu wanaofanya kazi katika sekta zisizo rasmi.” 

Kwa mantiki hiyo amesema “Kushikamana kwa pamoja kwa ajili ya maslahi ya kila mtu ndio njia pekee ya kujikwamua vyema na salama kutoka kwenye janga hili.” 

Katika siku hii ya kimataifa ya kutokomeza umasikini ambayo huadhimishwa kila mwaka Oktoba 17, ametoa wito wa kusimama Pamoja na kushikamana na watu wanaoishi katika umasikini wakati wote wa janga la COVID-19 na baada ya janga hilo.