Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kiu ya watoto kutaka kusoma imenipa nguvu ya kufundisha wakati wa COVID-19:Aylin Tufan 

Mwalimu nchini Ufaransa akifundisha watoto kupitia maandao. Elimu mandaoni ndio muarobaini wa kukabilia na changamoto za kufika shuleni wakati huu wa janga la COVID-19
ILO Photo/Marcel Crozet
Mwalimu nchini Ufaransa akifundisha watoto kupitia maandao. Elimu mandaoni ndio muarobaini wa kukabilia na changamoto za kufika shuleni wakati huu wa janga la COVID-19

Kiu ya watoto kutaka kusoma imenipa nguvu ya kufundisha wakati wa COVID-19:Aylin Tufan 

Utamaduni na Elimu

Kutana na mwalimu kutoka nchini Uturuki anayesema janga la corona au COVID-19 lilimvunja moyo na kumkatisha tamaa, lakini ari ya wanafunzi wake ambao asilimia kubwa ni wakimbizi kutoka kutoka Syria ilimpa nguvu ya kuendelea kufundisha.

Mjini Mersin uturuki 

Nattss….jina langu ni  

Aylin Tufan mwenye umri wa miaka 25 akijinadi kuwa ni mshauri nasaha wa masuala ya kisaikolojia na mwalimu ambaye kwa zaidi kwa mwaka mmoja sasa amekuwa akifundisha katika shule za umma. “Wanafunzi wangu ni wa kati ya umri wa miaka 10 na 18 na asilimia kubwa ni watoto wakimbizi na barubaru kutoka Syria. Wengi wa watoto hawa wamepitia changamoto nyingi kama vile ubaguzi, ajira ya watoto na ndoa za utotoni.”

Mwalimu Aylin ambaye ni mmoja wa mashujaa wa elimu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF,  amasema janga la corona au COVID-19 liliongeza changamoto kwa watoto hawa, wazazi na walimu pia kwani shule zilifungwa , na wengi hawakuweza kusoma, yeye na waalimu wenzie walifanya kila liwezekanalo kuhakikisha masomo yanaendelea kwa watoto hawa kupitia video walizorekoni na kuziweka mtandaoni kwenye Youtube “Pale ambapo wanafunzi wetu wenye simu za rununu walipotuambia hawawezi kuingia mtandaoni hawana intaneti, mimi na waalimu wenzangu tulichukua hatua kuwasaidia kununua vifurushi vya intaneti na tulihakikisha wanafuatilia masomo hayo.” 

Aylin anasema kilichomsukuma ni,“Kiu ya wanafunzi wangu kupata elimu, naweza kusema ari yao ya kujifunza na kupata elimu ilizkuwa ni sababu kubwa ya kunitia moyo kuendelea na juhudi zangu za kufundisha wakati wa janga hili.” 

Anasema ili watoto wasome wanahitaji waalimu hivyo wito wake ni kuwasaidia waalim na kuwawezesha ili waendelee kufundisha wakati huu wa COVID-19 kwa kuwekeza katika elimu.