Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uzoefu wa UNAIDS katika VVU/UKIMWI watoa mwongozo wa kupunguza unyanyapaa wakati wa COVID-19 

 “Unyanyapaa husababisha habari potofu na ubaguzi. Hiyo inatuzuia kusonga mbele. " Clara, 23, Hispania
© UNICEF/@witchtropolis
“Unyanyapaa husababisha habari potofu na ubaguzi. Hiyo inatuzuia kusonga mbele. " Clara, 23, Hispania

Uzoefu wa UNAIDS katika VVU/UKIMWI watoa mwongozo wa kupunguza unyanyapaa wakati wa COVID-19 

Afya

Kwa kutumia uzoefu wake wa miaka 40 ya kushughulikia ugonjwa wa UKIMWI, shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya UKIMWI, UNAIDS, limetoa mwongozo mpya kuhusu jinsi ya kupunguza unyanyanyapaa na ubaguzi wakati wa kushughulikia COVID-19. Mwongozo huo unategemea ushahidi wa hivi karibuni juu ya kile kinachofanya kazi kupunguza unyanyapaa na ubaguzi unaohusiana na Virusi Vya UKIMWI, VVU na unatumika kwa COVID-19. 

Tangu kuanza kwa janga la COVID-19, aina mbalimbali za unyanyapaa na ubaguzi vimeripotiwa ikiwemo ubaguzi dhidi ya mtu kutokana na taifa lake anakotoka ambapo ubaguzi huu ulielekezwa moja kwa moja kwa watu ambao walifikiriwa kuwa wao ndio walioleta COVID-19 katika nchi mbalimbali, mashambulizi kwa wahudumu wa afya na pia unyanyasaji kwa njia ya maneno n ahata mwili kuelekea kwa watu ambao wamepona ugonjwa wa COVID-19. Pia mashambulizi kwa watu ambao tayari walikuwa wanakabiliwa na unyanyapaa na unyanyasaji wakiwemo watu wanaoishi na VVU, watu wa makundi maalumu, wanaofanya biashara ya kuuza miili na pia wahamiaji.  

Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS Winnie Byanyima, amesema, “kufuatia hofu na kutokuwa na uhakika zinazojitokeza wakati wa janga, unyanyapaa na ubaguzi hufuata haraka. Unyanyapaa na ubaguzi hauna tija. Vinawaweka watu kwenye vurugu, unyanyasaji na kutengwa, vinawazuia watu kupata huduma za afya na vinazuia hatua za afya ya umma kudhibiti vimelea vyema.” 

Mwongozo huo wa takribani kurasa 24 uliopewa jina Kushughulikia unyanyapaa na ubaguzi katika kupambana na COVID-19 unazipa nchi mwongozo unaozingatia haki kupitia elimu, msaada, rufaa na hatua nyingine. Pia mwongozo huo unatoa suluhisho katika maeneo mengine sita mahususi ambayo ni  jamii,  

"Tunafahamu kinachofanya kazi na kisichofanya kazi, tunajua jinsi ya kubadilisha imani na tabia. Kwa miaka 30 iliyopita tumekuwa tukiongoza kwa mafanikio mapambano ya VVU, tukijenga uzoefu muhimu, maarifa na hekima njiani. Tunataka kutoa uzoefu huu ili kubadilisha maisha ya watu kuwa bora, na kutoa mchango wetu tofauti kushinda janga la COVID-19." Amesema Alexandra Volgina, Mratibu wa Programu, Ushirikiano wa kimataifa katika kuondoa aina zote za unyanyapaa na ubaguzi unaohusiana na VVU.