Skip to main content

COVID-19 yamlazimisha mwalimu kusaka kipato mbadala nchini Uganda

Martha Achok akikuza uelewa kuhusu jinsi ya kuzuia kusambaa kwa COVID-19 nchini Uganda.
UN Women /Aidah Nanyonjo
Martha Achok akikuza uelewa kuhusu jinsi ya kuzuia kusambaa kwa COVID-19 nchini Uganda.

COVID-19 yamlazimisha mwalimu kusaka kipato mbadala nchini Uganda

Utamaduni na Elimu

Leo ikiwa ni siku ya walimu duniani, ambayo mwaka huu inaadhimishwa kukiwa na changamoto kubwa kwa walimu na wanafunzi kufuatia janga la corona au COVID-19, huku Umoja wa Mataifa ukisema takriban wanafunzi bilioni 1.6 ambao ni zaidi ya wanafunzi wote duniani waliojiandikisha shule wameathiriwa na kufungwa kwa shule. 

Hata hivyo waalimu pia wamepata pigo kubwa wengine wakilazimika kutafuta njia mbadala ya kuweza kujikimu kimaisha baada ya sehemu zingine mishahara kutolipwa kwa wakati. Nchini Uganda mwandishi wetu John Kibego amezungmuza na mwalimu Scovia Ahuura wa shule ya sekondari ya Bukuumira jijini Hoima kuhusu jinsi gani anavyokabiliana na changamoto hizo zikiwemo za kiuchumi zilizoibuka baada ya shule kufungwa kutokana na COVID-19

(MAHOJIANO YA JOHN KIBEGO NA SCOVIA)