UN-HABITAT yachukua hatua kupambana na COVID-19 hata kwa wasio na makazi Kenya

5 Oktoba 2020

Ikiwa leo ni siku ya makazi duniani, kuwa na makazi bora imeelezwa hivi sasa kuliko wakati mwingine wowote ni suala la uhai na kifo hasa janga la corona  au COVID-19 likiendelea kusambaa duniani na watu wakitakiwa kusalia majumbani, lakini hatua hiyo haiwezekani hasa kwa wale ambao hawana wanapopaita nyumbani limesema shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UN-HABITAT.

Nchini Kenya shirika hilo limechukua hatua likihusisha vijana na kina mama kupambana na corona hata kwa watu wasio na makazi bora ikiwemo kufadhili vituo vya kunawa mikono na kushona barakoa kama wanavyosema washiriki wa harakati hizo Isaac Muasa na Pauline Wanjiku kutoka mitaa ya mabanda ya Kibera na Mathare walipozungumza na mwandishi wetu Jason Nyakundi

(MAHOJIANO NA JASON NYAKUNDI)

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud