Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Walimu wako mstari wa mbele kufundisha hata zama za sasa za COVID-19 

Wanafunzi kutoka shule ya msingi ya Minyinyi, nchini Tanzania na mwalimu wao ambaye anawafundisha kutumia kifaa cha kupima rutuba kwenye ardhi kwa ajili ya vipimo vya mbolea.
FAO Tanzania
Wanafunzi kutoka shule ya msingi ya Minyinyi, nchini Tanzania na mwalimu wao ambaye anawafundisha kutumia kifaa cha kupima rutuba kwenye ardhi kwa ajili ya vipimo vya mbolea.

Walimu wako mstari wa mbele kufundisha hata zama za sasa za COVID-19 

Utamaduni na Elimu

Kila mwaka, siku ya walimu duniani inatukumbusha dhima muhimu ya walimu katika kufanikisha elimu jumuishi na bora kwa watu wote. 

Hivyo ndivyo ulivyoanza ujumbe wa pamoja wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau kuhusu elimu, katika siku ya walimu duniani hii leo, siku inayotambuliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO

Wakuu wa mashirka hayo, lile la kuhudumia watoto, UNICEF, Henrietta Fore, UNESCO, Audrey Azoulay, la kazi, ILO, Guy Rider na Katibu Mkuu wa Educational International David Edwards, wamesema, hata hivyo mwaka huu, siku ya walimu dunani ina umuhimu wa kipekee kutokana na changamoto ambazo walimu wanakabiliana nazo wakati wa zama za sasa za janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19.” 

Wamesema kadri janga hili lilivyodhihirisha, walimu wana mchango mkubwa katika kuhakikisha kuendelea kwa kujifunza na wakati huo huo kusaidia afya ya akili na ustawi wa wanafunzi wao. 

“Kwa sababu ya COVID-19, takribani wanafunzi bilioni 1.6, zaidi ya asilimia 90 ya wanafunziwote duniani waiojiandikisha shuleni, wameathiriwa na kufungwa kwa shule. Janga la COVID-19 limeathiri pia zaidi ya walimu milioni 63, hivyo kuonesha udhaifu kwenye mifumo ya elimu na kuongezeka kwa ukosefu wa usawa na madhara yake kwa wale wakazi wa pembezoni,” umesema ujumbe wao wa pamoja. 

Viongozi hao wamesema katika janga la sasa, waimu wameonesha kama ambavyo wamekuwa wakidhihirisha mara kwa mara uongozi wao na ubunifu katika kuhakikisha kuwa katu kujifunza hakukomi na hakuna mwanafunzi anayeachwa nyuma. 

Walimu na kujituma 

Ulimwenguni kote, walimu wamefanya kazi iwe ni mmoja mmoja au kwa kikundi kusaka suluhu na kuweka mazingira mapya ya wanafunzi kujifunza na kuendelea na masomo yao. 

“Jukumu lao katika kuhakikisha shule zinafunguliwa ten ana kusaidia wanafunzi kurejea shuleni ni muhimu pia,” imesema hotuba hiyo. 

Hata hivyo wamesema hivi sasa wanafikiria zaidi ya COVID-19, na kushirikiana kujenga mnepo ili kuweza kushughulikia mapema janga la sasa na ya badayel. 

Viongozi hao hata hivyo wamekumbusha kuwa bila uwekezaji wa dharura, janga la kutojifunza linaweza kuibua janga kubwa aidi, “hata kabla ya COVID-19, zaidi ya nusu ya watoto wenye umri miaka 10 katika nchi za kipato cha kati zilizkuwa zinaelewa hali halisi. 

Ili kujanga nguvu kazi ya walimu yenye mnepo wakati wa majanga walimu wote lazima wapatiwe vifaa na stadi za teknolojia ya kisasa. 

Serikali yenyewe kwa upande wake ihakikishe uwepo wa miundombini ya kidijitali na mtandao wa intaneti kila pahali ikiwemo maeneo ya ndani zaidi. 

Viongozi hao wa UNESCO, UNICEF, ILO na Educational International wamesema serikali lazima zilinde usalama, afya na ustawi na ajira ya walimu na kuendelea kuboresha mazingira yao ya kazi na kujumuisha mashirika yote yanayohusisha walimu kwenye mikakati ya kujikwamua.