Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tukishikamana na kutumia nyezo tuliyonayo tutalishinda janga la COVID-19:UN 

Sampuli zikipimwa na wanasayansi katika Taasisi ya Jenner ya Chuo Kikuu cha Oxford ikiwa ni katika harakati za kutafuta chanjo dhidi ya virusi vya corona.
University of Oxford/John Cairns
Sampuli zikipimwa na wanasayansi katika Taasisi ya Jenner ya Chuo Kikuu cha Oxford ikiwa ni katika harakati za kutafuta chanjo dhidi ya virusi vya corona.

Tukishikamana na kutumia nyezo tuliyonayo tutalishinda janga la COVID-19:UN 

Afya

Umoja wa Mataifa leo umefanya mkutano wa ngazi ya juu kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa ukishirikisha wadau mbalimbali kupitia mtandao kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na kutumia nyenzo zilizopo kwa ajili utengenezaji wa chanjo dhidi ya janga la corona au COVID-19. 

Akifungua mkutano huo uliobeba kaulimbiu “kukaribia kulitokomeza janga la coronavirus">COVID-19” , Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameeleza ni kwa nini mkakati wa ACT-Accelerator ni muhimu sana katika kusongesha juhudi za kutengeneza na kusambaza vipimo, dawa na chanjo dhidi ya corona. 

“Ni kwa ajili ya maslahi ya kila nchi ya kitaifa na kiuchumi kufanyakazio pamoja ili kupanua wigo wa fursa za upimaji na matibabu na kuunga mkono upatikanaji wa chanjo kwa maslahi ya umma, chanjo ya watu ambayo inapaswa kupatikana kwa kila mt una kwa gharama nafuu, kila mahali na mkakati wa ACT-Acceletrator na kituo cha COVAX ndio chombo cha kutufikisha katika malengo hayo.” 

Amesisitiza kuwa fura ya nyenzo ya mchakato wa ACT na kituo chake cha COCAX ni mifano muafaka ya ushirikiano wa kimataifa kwa jail ya umma wote. 

Guterres amesema anatambua na kuthamini dola bilioni 3 zilizotolewa kuanza mchakato wa ACT-Accelerator lakini amesisitiza haja ya kuongeza ufadhili wa dola zingine bilioni 35 zinazohitajika kufadhili machakato huo. 

Amewahimiza viongozi wa dunia kwamba, “tunahitaji kufikiria kwa mapana zaidi. Ni wakati wa nchi kukusanya fedha kutoka kwenye miakati yao ya kupambana na janga hili na mipango ya kujikwamua. Kwa kusaidia wengine watakuwa wanajisaidia pia.Janga la COVID-19 linaugharimu uchumi wa dunia dola bilioni 375 kwa mwezi na ajira milioni 500 tangu lilipozuka.” 

Ameongeza kuwa ulimwengu ulioendelea umetenga matrilioni yad ola kupambana na athari za kiuchumi na kijamii za janga hili katika nchi zao.”kwa hakika tunaweza kuwekeza sehemu ndogo ya fedha hizo ili kukomesha kusambaa kwa janga hili kila mahali.” 

ACT-Accelerator mkakati wa kuchapuza fursa za upatikanaji wa fedha kupambana na COVID-19 ulizinduliwa mwezi April mwaka huu. Mkakati huu mpya lengo lake ni kuharakisha utengenezaji, uzalishaji na usambazaji wa sawa wa vifaa vya upimaji, matibabu na chanjo dhidi ya COVID-19. 

Na unawaleta pamoja wadau wote zikiwemo serikali, wanazuoni, kampuni binafsi, asasi za kiraia, mashirika ya hisani na mashirika ya kimataifa ya afya. 

Kwa kupitia mkakati huo ambao sasa unajumuisha nchi 156 sawa na theluthi mbili ya watu wote duniani utaruhusu shughuli za kiuchumi kuanza katika kiwango cha kimataifa kwa muda mfupi. Na Zaidi yah apo utaziwezesha nchi za kipato cha wastani na cha chini kupokea vipimo milioni 120 vya COVID-19 vyenye ubora wa hali ya juu lakini kwa gharama nafuu “Kwa kuwekeza katika ACT-Accelerator utafanya kujikwamua kwa kila nchi kutokana na janga hili kuwa rahisi na karibu.” Amesema Bwana Guterres.