Nadia Murad ashutumu ukosefu wa nia ya kumaliza ukatili wa kijinsia unaotumika kama mbinu ya vita. 

Nadia Murad akihutubia kwa njia ya video, kuhusu mapambano dhidi ya ukatili wa kingono unaotumika kama silaha ya kivita.
UN Photo/Rick Bajornas)
Nadia Murad akihutubia kwa njia ya video, kuhusu mapambano dhidi ya ukatili wa kingono unaotumika kama silaha ya kivita.

Nadia Murad ashutumu ukosefu wa nia ya kumaliza ukatili wa kijinsia unaotumika kama mbinu ya vita. 

Sheria na Kuzuia Uhalifu

Katika mazingira ambayo mwanamke mmoja kati ya wanawake watatu duniani kote ameathiriwa  na unyanyasaji wa kijinsia, uhalifu ambao unapaa zaidi kwa asilimia 200 katika mazingira ya mizozo, mshindi wa tuzo ya Nobel Nadia Murad amezishutumu serikali za ulimwengu kwa kushindwa kutoa rasilimali zinazohitajika kutengeneza mabadiliko ya kweli kwa jamii ambazo zimeathiriwa.   

"Tuna uwezo wa kutoa rasilimali kwa jamii zilizoharibiwa na vurugu. Tunakosa nia ya pamoja ya kisiasa kufanya hivyo." Bi Murad, ambaye pia anahudumu kama Balozi mwema wa Umoja wa Mataifa, amesema.  

Akizungumza hii leo katika tukio lililofanyika kwa njia ya mtandao likipewa jina #EndSGBV lililoandaliwa na Muungano wan chi za kiarabu UAE, Norway na Somalia kandoni mwa mjadala wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Bi. Murad, ambaye katika mwaka 2018 yeye pamoja na daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake Denis Mukwege wa DR Congo, walitunukiwa tuzo ya amani ya Nobel kwa juhudi zao za kutokomeza matumizi ya unyanyasaji wa kijinsia kama silaha ya vita. 

"Tunapaswa tuangalie kwa kina kile tulichofanya vizuri, ambapo tunaweza kujivunia kwa sababu tumepata tofauti ya kweli. Lakini pia, kuwa waaminifu na uwazi mahali ambapo tumekosa fursa za kukomesha unyanyasaji wa kijinsia na kweli kuwasaidia waathiriwa. ” Amesisitiza mwanaharakati huyo. 

Tuwahusishe manusura 

Bi Mradi amesema katika maeneo ambayo yalikuwa na migogoro kama Iraq, manusura wanapaswa wachukue jukumu kubwa katika mchakato wa ujenzi wa amani. “Manusura wanafahamu kile wanachokihitaji ili kupona na kurejea katika hali yao.” Kwa hivyo jitihada za kuwashirikisha katika kila ngazi ya kupona kwao, zitawapa nguvu.