Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunapoadhimisha siku ya utalii , tuwakumbuke watu wa vijijini:Guterres

Watalii nchini India wakitumia usafiri wa tembo kupanda katika eneo la mnara wa Amber nje kidogo ya Jaipur.
Eric Ganz
Watalii nchini India wakitumia usafiri wa tembo kupanda katika eneo la mnara wa Amber nje kidogo ya Jaipur.

Tunapoadhimisha siku ya utalii , tuwakumbuke watu wa vijijini:Guterres

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesihi dunia katika wakati huu wa changamoto kubwa zinazoikabili dunia likiwemo janga la corona au COVID-19 ni muhimu kutowasahau watu wanaoishi vijijini katika ahadi ya maendeleo endelevu au SDGs. 

Kupitia ujumbe wake wa siku ya utalii duniani Antonio Guterres amesema , ikiwa ni miaka 40 sasa tangu kuanza kuadhimishwa siku ya hii mambo mengi yamebadilika na mahitaji ya kusafiri yameongezeka sana, lakini pia dunia imefunguka zaidi na kuruhusu watu wengi kuliko wakati mwingine wowote kuisoma dunia katika sehemu mbalimbali na utamaduni tofauti. 

Ameongeza kuwa leo hii utalii umewekwa bayana katika ajenda ya Umoja wa Mataifa ya 2030 ya maendeleo endelevu kama injini ya kusongesha mafanikio, kulinda sayari yet una kuweka msingi kwa ajili ya amani na kuwaelewa watu mbalimbali.  

“Mamilioni ya watu kote duniani wanategemea utalii kama chanzo cha kipato, hususani wanawake na vijana. Watu ambao pengine wangebakizwa nyuma sasa wamepata ajira zenye hadhi na fursa ya kujenga maisha bora, shukrani kwa sekta ya utalii na fursa zake za kipekee.” 

Guterres amesema hata hivyo janga la COVID-19 limeleta athari kubwa katika sekta ya utalii. Hivi sasa ajira milioni 120 ziko hatarini na athari hizo zinaweza kusababisha hasara ya kati ya asilimia 1.5 na 2.8 ya pato la dunia (GDP) 

Amesema nah ii itawaathiri zaidi nchi zisizojiweza na zilizo hatarini zikiwemo nchi zinazoendelea za visiwa vidogo , nchi zenye maendeleo duni na mataifa mengi ya afrika ambako utalii unawakilisha kati ya asilimia 30 na 80 ya bidhaa zinazosafirishwa nje. 

Kwa mantiki hiyo Katinu Mkuu amehimiza kwamba “wakati tukijiandfaa kujikwamua kutoka kwenye janga hili kufufua tena utalii salama ni muhimu hususan kwa maendeleo ya vijijini ambayo ndio mada kuu ya maadhimisho yam waka huu ya siku ya utalii duniani. Tuna fursa kubwa ya kubadili uhusiano uliopo baina ya sekta ya utalii na na watu, mazingira, mabadiliko ya tabianchi na uchumi. Ni lazima tuhakikishe kwamba kuna ugawanaji sawa wa faida za utalii na kusongesha mchakato wa mabadiliko kuingia kwenye uchumi wa utalii usioharibu na kuchafua mazingira na wenye mnepo.” 

Pamoja na hayo ni muhimu kutoa fursa kwa watu kwani utalii unaweza kuwa na jukumu kubwa sana katika kulinda utamaduni wetu wa kipekee na kulinda bayoanuai na mfumo mzima wa Maisha ambao unaturuhusu kendelea kuwepo. 

Kwa mantiki hiyo Katibu Mkuu amesema “katika mwaka huu wa changamoto kubwa hebu na tujikite katika umuhimu wa utalii kwa watu wanaoishi vijijini , ili tuweze kutimiza ahadi ya malengo ya maendeleo endelevu ya kutomuacha yeyote nyuma.”

Siku ya utalii duniani huadhimishwa kila mwaka Septemba 27.