Dawa za uzazi wa mpango zapaswa kupatikana hata wakati wa COVID-19:UN

26 Septemba 2020

Fursa ya upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpango ni haki ya binadamu inayolindwa chini ya sheria za kimataifa na nchi ni lazima ziendelee kuhakikisha huduma hiyo inapatikana hata wakati wa janga la corona au COVID-19, wamesema wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa. 

Haki ya afya ya uzazi 

Katika kuadhimisha siku dawa za uzazi wa mpango duniani COVID-19 limekuwa na athari kuibwa katika huduma ya uzazi wa mpango. Uzalishaji wake umepunguzwa na usambazaji wake imevurugwa. Vituo vya afya vimefungwa au kuna huduma ndogo hususan katika nchi ambazo zina rasilimali ndogo na wanawake na vigori hawawezi kuwafikia wahudumu wa afya wenye ujuzi. 

Wamefafanua kwamba “haki ya afya ya uzazi inajumuisha uhuru wa wanawake kuamua endapo wapate ujauzito ama la, ni watoto wangapi wanataka kuwa nao na mimba zao zitofautiane kwa muda gani.” 

Pia haki hiyo wamesema inaweka jukumu kwa nchi wanachama kutoa dawa muhimu zilizopo kwenye orodha ya shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO ambazo ni Pamoja na dawa za uzazi wa mpango. 

“Ili kutimiza ndoto ya haki nii kila mtu lazima awe na fursa ya elimu ya kisayansi ya afya ya uzazi ambajo inapaswa kujumuishwa kwenye mitaala ya shule pamoja na njia salama, za wakati, zinazofanya kazi, za gharama nafuu na zinazokubalika za uzazi wa mpango ambazo watazichagua.” 

Njia hizo wamesema ni Pamoja na taarifa za kisanyansi zinazotolewa bila upendeleo, fursa ya kufanya maamuzi wakiwa na taarifa kamili, chaguo la ushauri nasaha, dawa za kisasa za uzazi wa mpango za muda mfupi na zile za muda mrefu na njia nyingine kama vile huduma ya uzazi wa mpango ya dharura. 

Wataalam hao wamesisitiza kwamba vikwazo vilivyowekwa kwa ajili ya kupambana na janga la COVID-19 visimzuwie yeyote kupata taarifa wanazohitaji na fiursa ya wakati muafaka ya huduma kwenye vituo vya afya. 

Vituo hivyo ni vile ambavyop bvinatoa huduma muhimu kama vipimo na kupambana na magonjwa ya zinaa, kutoa msaada kwa waathirika wa ukatili wa kingono au ubakaji, utoaji mimba salama na kutoa huduma ya mipira ya kiume nay a kike au njia zingine za uzazi wa mpango. 

Ni muhimu huduma kuwafikiwa wanaobaguliwa 

Wataalam wa haki za binadamu wamesisitiza kwamba ni muhimu hususan kuhakikisha fursa inapatikana kwa wale walio hatarini au ambao kihistoria wanabaguliwa kama vile wasichana vigori, wanawake wahamiaji, wanawake wenyen ulemavu, wakazi wa mitaa yam abanda, wakimbizi, watu wa LGBT na jamii za watu waliobadili jinsia, Pamoja na wanawake waliotoka kujifungua. 

Wamekumbusha kwamba maamuzi na fursa za huduma ya uzazi wa mpango ni muhimu kwa afya ya uzazi ya watu binafasi na pia katika utimizaji wa malengo ya maendeleo endelevu  kuhusu usawa wa kijinsia na afya na ustawi hususan kwa wale wanaolenga kuhakikisha halki ya huduma ya afya ya uzazi wa mpango kwa wote na kupunguza vifo vya kina mama wakati wa kujifungua. 

“Katika siku dawa za uzazi wa mpango duniani Septemba 26 na siku ya kimataifa ya utoaji mimba salama 28 Septemba , tunatoa wito kwa mataifa yote kutimiza jukumu lao muhimu la kuhakikisha kuna ongezeko la fursa ya njia za kisasa na botra za huduma za uzazi wa mpango , zisizo na unyanyapaa na zinazotokana na misingi ya taarifa sahihi. 

 

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter