Hakuna muda wa kupoteza mabadiliko ya tabianchi ni janga la dharura:UN  

24 Septemba 2020

Mgogoro wa mabadiliko ya tanianchi ni dharura ya kimataifa inayohitaji harua za haraka kwani hakuna muda wa kupoteza nah atua zisipochukuliwa sasa basi dunia itashuhudia zahma si ya kawaida umeonya leo Umoja wa Mataifa. 

Onyo hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika majadiliano ya ngazi ya juu kandoni mwa mjadala wa Baraza Kuu yanayohusu malengo ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi. 

Katika majadiliano hayo ambayo yamefanyika kwa njia ya mtandao, Katibu Mkuu ameonya kuhusu ongezeko la matukio ya hali mbaya ya hewa kuanzia ya moto wa nyika hadi mafuriko ya kihistoria. 

Akitaja ripoti ya hivi karibuni ya shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO ikiainisha viwango vya kihistoria vya gesi ya hewa ukaa kutokana na mafuta ya kiskuku na moto wa nyika mwaka 2019 ambapo viwango vimekuwa asilimia 62% zaidi ya ilivyokuwa mwaka 1990. 

Mipango mkakati 

Katibu Mkuu ametakja kuwa miaka mitano baada ya kutiwa saini mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi ni miaka iliyokuwa na joto la kupindukia katika historia ya binadamu kwa mujibu wa shirika la masuala ya anga la NASA. 

Hivyo Guterres ametaja vipaumbele vitatu vya haraka kwa viongozi wa dunia , serikali, makampuni, wafadhili, asasi za kiraia na vijana . 

Mosi ni kwamba mipango ya kujikwamua kutoka kwenye janga la COVID-19 lazima iwe endelevu na inayoshughulikia mabadiliko ya tabianchi. 

Pili katibu Mkuu amesema ni lazima kulinda uchumi na jamii kwa kuchukua hatua kutokana na takwimu za kisayansi. 

Tatu ni kuhakikisha kwamba wat una jamii zilizohatarini wanapewa kipaumbele. 

Ametoa wito kwa nchi kufikiria hatari za mbadiliko ya tabianchi katika maamuzi yake yote ya kifedha na kisiasa. 

Pia amesema mikakati ya kujikwamua na janga la COVID-19 inahitaji kuzingatia suala la upunguzaji hewa ukaa katika uchumi wa kimataifa. 

Kwa Katibu Mkuu kuhamia kwenye nishati jadidifu ni muhimu na kutaongeza ajira zaidi kuliko kuendelea na mafuta kiskuku. Na uwezekano wa uchumi endelevu wa blub ado hakujadadisiwa. 

Hatua za mabadiliko ya tabianchi 

Guterres amekumbusha mkutano wa mwaka jana wah atua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.  Amesema katika mkutano huo viongozi wa serikali kuu na mashinani, asasi za kiraia, benki na makampuni walikuja pamoja kuongoza hatua halisi kuelekea utokomezaji kabisa wa hewa ukaa kupitia uchumi unaijali mazingira ifikapo mwaka 2050. 

Anatarajia kwamba mkutano wa kimataifa wa viongozi, makampuni na asasi za kiraia utakaofanyika desemba 12 kuadhimisha miaka mitano ya mkataba wa Paris utaendelea kusongesha dhamira hiyo ya hatua dhidi ya mabnadiliko ya tabianchi. 

Ahadi kutimiza lengo 

Guterres pia amesisitiza kwamba dharura ya mabadiliko ya tabianchi imefurutu ad ana hakuna muda wa kupoteza.  

Kwa upande wake jawabu la changamoto hii ni “maamuzi ya busara, ya haraka na mshikamano wa Pamoja kwa ajili yah atua miongoni mwa mataifa. 

Wito mwingine kutoka kwa mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ni ahadi ya mara moja ya kuchukua hatua Madhubuti ambazo zitaweka msingi wa dunia kwa ajili ya afya, usalama na mafanikio kwa wote. 

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud