Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tunakaribisha ushirikiano utakaosaidia juhudi zetu za kupambana na ugaidi Msumbiji-Rais Nyusi

Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji akihutubia mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA75 kwa njia ya video.
UN Photo/Eskinder Debebe)
Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji akihutubia mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA75 kwa njia ya video.

Tunakaribisha ushirikiano utakaosaidia juhudi zetu za kupambana na ugaidi Msumbiji-Rais Nyusi

Amani na Usalama

Rais wa Msubiji Filipe Nyusi akihutubia mjadala wa wazi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, kwa njia ya video iliyorekodiwa, hii leo Jumatano amesema kuwa mapigano katika Msumbiji tayari yameua zaidi ya watu 1,000 na kwamba vikosi vya usalama vinajibu mashambulizi ya watu wenye itikadi kali za Kiislamu katika mkoa wa Cabo Delgado na sehemu za maeneo ya Manica na Sofala pia zinaathiriwa na watu kujihami kwa silaha. 

Rais Nyusi ameyahusisha mashambulizi ya maeneo ya Manica na Sofala na "watu wanaodaiwa kuwa wapinzani kutoka chama kikubwa zaidi cha upinzani nchini Msumbiji, Renamo.” 

Uhalifu wa kupangwa 

Kwa mujibu wa Rais Nyusi, serikali inakabiliana na hali hiyo kwa uthabiti na kwa msaada wa wadau wengine kama shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa akikumbushia kuanzia nchi yake ilipopigwa na kimbunga Idai. Sasa wimbi jipya kutokana na vurugu limewafanya watu wengi kukimbilia katika nchi jirani, Tanzania.   

“Magaidi wanaua watu vibaya, wanafurusha watu, kuharibu nyumba na miundombinu, wanateka mali za jamii na kuwaweka watoto na wanawake kizuizini. Watu takribani 250,000 wamefurushwa makwao.” Amesema Rais Nyusi.

Watoto wakiwa katika kambi ya Taratara mkoani Cabo Delgado
UN Photo/Eskinder Debebe)
Watoto wakiwa katika kambi ya Taratara mkoani Cabo Delgado

 

Asante Umoja wa Mataifa 

Kwa mujibu wa Rais Nyusi ni kuwa matukio ya mashambulizi hayo ni yana uhusiano na uhalifu wa kimataifa wa kupangwa. Aidha ametumia nafasi hiyo kushukuru kwa msaada wa Umoja wa Mataifa pamoja na Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo, kwa kusaidia kukabiliana na changamoto hiyo ya usalama nchini Msumbiji. Kulingana na Filipe Nyusi, vitu kadhaa vyenye silaha vina uhusiano na uhalifu wa kimataifa uliopangwa.  

Bwana Nyusi amesema kwa kutambua kuwa vitendo vya kigaidi ambavyo nchi yake imeathiriwa vina uhusiano na makundi ya kimataifa ambayo yanahusika na uhalifu wa kupangwa, “tumetafuta kushughulikia jambo hili kwa kushirikiana nan chi nyingine na mashirika ya kikanda na ya kimataifa. Katika muktadha huu, tunakaribisha mipango yote na ushirikiano ambao utasaidia sana katika kusaidia juhudi zetu zinazoendelea za kupunguza vitendo vibaya vya magaidi katika nchi yetu. Kama sehemu ya utekelezaji wa Mkataba wa amani na upatanisho kati ya serikali na RENAMO, tunatekeleza ugawanyaji wa madaraka na mchakato wa Kutokomeza silaha, na pia mtangamano.”