Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujira sawa uwe kitovu cha kujikwamua kutoka kwenye COVID-19:EPIC/UN

Mfanyakazi mhamiaji akishona nguo katika kiwanda Magharibi mwa Thailand. Wakifanya kazi zaidi ya saa 12 kwa siku, pamoja na malipo ya muda wa ziada, bado wanapata malipo kidogo chini ya kiwango cha chini cha ujira wa siku.
UN Women/Piyavit Thongsa-Ard
Mfanyakazi mhamiaji akishona nguo katika kiwanda Magharibi mwa Thailand. Wakifanya kazi zaidi ya saa 12 kwa siku, pamoja na malipo ya muda wa ziada, bado wanapata malipo kidogo chini ya kiwango cha chini cha ujira wa siku.

Ujira sawa uwe kitovu cha kujikwamua kutoka kwenye COVID-19:EPIC/UN

Wanawake

Katika maadhimisho ya kwanza ya siku ya kimataifa ya malipo sawa, muungano wa kimataifa kuhusu malipo sawa EPIC na mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo linalohusika na masuala ya wanawake UN Women na shirika la kazi duniani ILO yametoa wito wa hatua madhubuti kuchukuliwa kutimiza ndoto hiyo ya malipo sawa. 

Kupitia taarifa yao ya pamoja iliyotolewa leo mashirika hayo yametoa wito kwa viopngozi wa dunia kuchukua hatua za lazima na kuhakikisha usawa katika malipo unakuwa kitovu cha juhudi za kujikwamua kutoka kwenye janga la corona au COVID-19 kote duniani. 

Ukiongozwa na ILO. UN Women na OECD muungao wa ujira sawa EPIC umewaleta pamoja wadau na wataalam mbalimbali ili kuzisaidia serikali, waajiri, wafanyakazi na mashirika yao kupiga hatua na mchakato wenye mpangilio maalum ili kufikia usawa katika malipo kwa wanawake na wanaume kila mahali duniani. 

COVID-19 imeongeza shinikizo 

Taarifa hiyo ya pamoja imesema janga la COVID-19 limeanika wazi kwamba jamii zimejengwa katika muktada wa kutothaminiwa ipasavyo au mara nyingu kutolipwa inavyostahili kwa kazi nyingi zinazofanywa na wanawake na wasichana. 

“Wanawake ni asilimia 70 ya wafanyakazi wote wa afya duniani na wamekuwa msitari wa mbele kufanyakazi kama wahudumu muhimu, viongozi wa kijamii, walezi na wahudumu wa ustrawi wa jamii. Kanbnla ya janga la COVID-19 wanawake kwa wastan walikuwa wakifanya kazi za kutoa huduma bila malipo mara tatu zaidi ya wanaume na majukumu hayo yameongezeka zaidi tangu kuzuka kwa COVID-19 hasa ukizingatia shule na huduma za malezi ya Watoto zimefungwa, huku mahitaji ya kuhudumia wazee yakiongezeka.” 

Wakati huu wa janga la COVID-19 wanawake walio katika soko la ajira wameathirika vibaya kwa mdororo wa muda mfupi wa kiuchumi uliosababishwa na janga hilo. 

Sekta nyingi ambazo zinategemea huduma kwa wateja ambazo nyingi huajiri wanawake mathalani mahoteli, za chakula na vinywaji na huduma za rejareja kwa wateja zimeathirika san ana changamoto za kiuchumi zilizoletwa na janga hilo.

Zaidi ya hapo wanawake mara nyingi wanajikuta katika hali mbaya kwenye ajira za sekta zisizo rasmi ukilinganisha na wanaume kama vile wafanyakazi wa majumbani, ngazi ya chini ya wahudumu wa majumbani katika mnyororo wa usambazaji wa kimataifa au kama wafanyakazi wachangiaji wa familia  na hii inamaanisha wana ulinzi mdogo sana dhidi ya kufukuzwa kazi, malipo ya ugonjwa au fursa za hifadhi ya jamii. 

 Ahadi ya viongozi wa dunia 

Katika maadhimisho haya ya kwanza kabisa ya siku ya kimataifa ya malipo sawa, vipongozi wa dunia wameahidi kuchukua hatua madhubuti kupunguza pengo hilo katika malipo. 

EPIC imetoa wito kwa serikali, waajiri, wafanyakazi na mashirika yao, sekta binafsi, asasi za kiraia na wanazuoni kuhakikisha kwamba wanawake hawaishii kupoteza ajira na kupunguziwa kipato. 

Hafla ya maazimisho hayo mbali ya mpiga debe mkubwa wa kuchagiza malipo sawa  kepteni wa timu ya taifa ya soka ya wanawake ya marekani Megan Raoinoe  imehuduriwa pia na Guy Ryder mkuu wa ILO, Phumzile Mlambo-Ngcuka mkuu wa UN Women, Jose Angel Gurria Katibu mkuu wa OECD, Rais wa Iceland Guoni Johannesson na katibu mkuu wa shirika la kimataifa la wafanyakazi Guoni Johannesson. 

 

TAGS: EPIC, ILO, UN Women, OECD, Siku za UN, malipo sawa