Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukiukwaji wa haki za binadamu bado unaendelea Burundi licha ya serikali mpya:tume ya uchunguzi 

Doudou Diène, rais wa tume ya uchunguzi Burundi
Picha: UN/Jean-Marc Ferré
Doudou Diène, rais wa tume ya uchunguzi Burundi

Ukiukwaji wa haki za binadamu bado unaendelea Burundi licha ya serikali mpya:tume ya uchunguzi 

Haki za binadamu

Matiumaini yaliyoletwa na uchaguzi wa Rais mpya Evariste Ndayishimiye na kufungua ukurasa mpya nchini Burundi sasa bado ni kitendawili kukiwa hakuna hatua kubwa sana zilizopigwa katika suala la haki za binadamu imesema tume ya Umoja wa Mataifa ya uchunguzi kuhusu haki za binadamu katika taifa hilo la maziwa makuu. 

Kwa mujibu wa taaifa iliyotolewa leo mjini Geneva Uswis na wachunguzi wa tume hiyo uteuzi unaofanyika na maazimio yanayotangazwa hadharani na serikali ya Burundi“yanatia hofu zaidi badala ya ahadi za matumaini”. 

Tume hiyo imetoa onyo jipya kuhusu kuendelea kwa ukiukaji wa haki za binadamu na ukwepaji wa sharia nchini Burundi, tangu kufariki dunia kwa Rais wa zamani wan chi hiyo Pierre Nkurunziza ambaye aligombea awamu ya tatu mwaka 2015 hatua ambayo ilionekana na upinzani kwenda kinyume na katiba. 

Karika ripoti yao tume hiyo ya haki za binadamu Burundi iliyoitishwa na Baraza la Haki za Binadamu imesema“kumekuwa na hatua ndogo sana tangu Rais Evariste Ndayishimiye aingie madarakani mwezi Juni.” 

Machafuko wakati wa uchaguzi 

Mmoja wa wajumbe wa tume hiyo ya uchunguzi Francoise Hampson ameelezea Ushahidi wa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu ikiwemo mauaji, utesaji na ukatili wa kingono. 

“Katika wiki za hivi karibuni kumeendelea kuwepo na mauaji, watu wameendelea kushikiliw na kuwekwa rumande na wengine wameendelea kutoweka. Hivyo kiasi inashangaza kwamba hali inaendelea kama ilivyokuwa ingawa uchaguzi umemalizika na hili ni suala linalotutia hofu kubwa.” 

Katika mkutano na waandishi wa Habari kwa njia ya mtandao mwenyekiti wa tume hiyo ya uchunguzi Doudou Diene ameonya kwamba“kubadilika kwa sera, uteuzi na taarifa zinazotolewa kwa umma na serikali mpya ya Burundi vinaonyesha sababu kubwa za kuwa na hofu na onyo kuliko ilivyotarajiwa.” 

Ameongeza kuwa nah ii ni kwa sababu vyeo muhimu katika serikali mpya vimejumuisha watu ambao wamebainika kutekeleza ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu katika utawala uliopita na ambao wanakabiliwa na vikwazo vyua kimataifa. 

Uteuzi wa kijeshi 

Zaidi yah apo asilimia kubwa ya uteuzi mpya uliofanywa ni watu kutoka jeshini amesema bwana. Diene huku hali ya kutowafikisha wakiukati wa haki za binadamu kwenye mkono wa sharia ndani ya nchi ikiendelea. 

Tume hiyo katika uchunguzi wake pia imebaini kwamba hali ya haki za binadamu nchini Burundi bado ni tete na inasalia katika hatari ya kudorora zaidi hata baada ya kufanyika uchaguzi mkuu wa 2020. 

Hili linaungwa mkono na matukio kadhaa ya kiusalama yaliyiotokea hivi karibuni na“Imbonerakure ambalo ni tawi la vijana wa chama tawala katika serikali kuendelea kudhibiti maeneo ya umma . Wanajifanya kama mawakala waliojitenga wa usalama katika maeneo mengin ya vijijini”na wachunguzi wamesema kulikuwa na kuzagaa kwa kauali za chuki wakati wa uchaguzi. 

Na hii inajumuisha kauli za uchochezi zenye mrengo wa kikabnila ambazo zimeendelea kuwa nyenzo ambayo inaweza ikatumika na mamlaka wakati wanaoona inafaa kisiasa. Wamesema wajumbe wa tume hiyo. 

Watoto wanalengwa 

Katika ripoti yao ambayo ni ya nne nay a mwisho kabla ya muda wa kazi yao kufikia ukomo wakati wa kikao hiki cha Baraza la Haki za Binadamu , wachunguzi hao pia walijikita na ukiukwaji mkubwa uliotekelezwa dhidi ya Watoto walio na umri wa chini ya miaka 18 ambao ni zaidi ya watu wote wa Burundi. 

Mjumbe mwingi wa tume hiyo Lucy Asuagbo amesema “wakati mwingine Watoto na vijana barubaru walikuwa wanalenghwa maksudi, walikuwa wakishinikizwa kuingia katika tawi la vijana la chjama tawala la Imbonerakure na wakati mwingine walikuwa wakiuumia wakati watu wa familia zao walipokuwa wakilengwa. Tuna hofu kubwa juu ya athari za machafuko yam waka 2015 kwa mustakabali wa Burundi, na hasa athari za muda mrefu za mgogoro huo kwa watoto.” 

Mapendekezo ya tume 

Miongoni mwa mapendekezo ya tume hiyo ya uchunguzi ni kwamba wameitaka serikali kuwaachilia mara moja watetezi wa haki za binadamu wanaoshikiliwa , pamoja na waandishi wa Habari na wafungwa wa kisiasa. 

Pia wameelezea hali ya ubadhilifu na umasikini unaoghubika asilimia 74 ya watu wa Burundi.“Kiwango cha ufisadi kimesambaa hivyo kila shirika, kampuni au watu wanaoleta ufadhili Burundi wanapaswa kuwa makini sana “amdesema Bi. Hampson. 

Ripoti hiyo itawasilishwa rasmi kwenye Baraza la Haki za binadamu Jumatano ya 23 Septemba.