Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni jinsi gani ya kuokoa baioanwai ya dunia? Sehemu nane za vipaumbele.

Mlima Kilimanjaro ulioko Tanzania
World Bank/Curt Carnemark
Mlima Kilimanjaro ulioko Tanzania

Ni jinsi gani ya kuokoa baioanwai ya dunia? Sehemu nane za vipaumbele.

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Upotevu wa bioanuwai umefikia rekodi ya viwango vya juu. Hekta bilioni mbili za ardhi zimepoteza rtuba yake. Zaidi ya aina milioni moja za wanyama na mimea katika sayari dunia viko katika hatari ya kutoweka. Watu wanazidi kuwa hatarini zaidi kwa vitisho vipya vya kibailojia kama vile janga la virusi vya corona. Hiyo ni sehemu ya toleo la tano la ripoti kuhusu bioanuwai ya dunia, ripoti ambayo imetolewa jumanne ya leo.

Ripoti inatathimini mafanikio ya utekelezaji wa Mpango mkakati kwa ajili ya bioanuwai katika mwaka 2011 hadi 2020.

Ripoti imeandaliwa na wataalamu kutoka katika Kongamano la utofauti wa bioanuwai. Wanaeleza kuwa kati ya malengo 20 yaliyowekwa, ni sita tu kati ya hayo ambayo yamefikiwa lakini hayo si matokeo mabaya, wakionesha kuwa juhudi za pamoja kulinda baioniwai zinasaidia kuokoa viumbe vyote.


“Kwa hivyo, katika miongo mitatu iliyopita, takribani aina 50 za ndege na Wanyama ambao walikuwa hatarini kupotea, zimeokolewa au kuhifadhiwa na 25 miongoni mwazo, katika muongo mmoja wa mwisho. Kwa mfano wanyama wadogo waitwao Black-footed ferrets wanaopatika katika Amerika pekee, wamehifadhiwa, ikikumbukwa kuwa walikuwa wamewekwa katika ‘kitabu cha chekundu cha takwimu’ tangu mwishoni mwa miaka ya 1960 kuwa wako hatarini kutoweka.” Ripoti imeeleza.


Wataalamu wameeleza pia kwamba karibu theluthi ya mashamba yote duniani takribani mashamba milioni 163 yanatumia njia endelevu za kilimo. Kiwango cha ukataji misitu kimepungua kwa asilimia 33. Hekta 22 za ardhi hivi sasa ziko katika kurejeshwa katika hali yake. 


Wataalamu wanasisitiza kuwa takwimu zote hizo zinaonesha kuwa hali ni ya kutia matumiani na jumuiya ya kimataifa inatakia kuongeza juhudi maradufu ili kuhifadhi na kuilinda bioanwai. Wataalamu hao wameainisha maeneo manane ya vipaumbele kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi katika eneo hili la utunzaji bioanwai.

Sehemu nane za vipaumbele.


Mosi, kulinda ardhi na misitu, ikiwemokudhibiti mmomonyoko wa udongo na kurejesha mfumo wa asili wa misitu.    


Pili, mabadiliko katika njia za kilimo kwa kutumia njia bora za kilimo zinazofuata mifumo ya asili ili kuboresha tija na huku ikipunguza athari mbaya kwenye baioanwai. 


Tatu, kufanya mabadiliko ya ulaji ikiwemo kuhamasisha maisha ya ulaji unaozingatia afya na umuhimu wa kula vyakula vya mimea zaidi kuliko nyama. 


Nne, kurejesha mzunguko wa ikolojia halisi ya baharini na kuendeleza ufugaji wa samaki. 

Vikundi vya samaki wa Trevally katika visiwa vya Solomon.
Coral Reef Image Bank/Tracey Jen
Vikundi vya samaki wa Trevally katika visiwa vya Solomon.

 


Tano, matumizi ya njia endelevu katika ujenzi mijini na utengenezaji wa miundombinu rafiki kwa mazingira.  


Sita, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, ikiwemo kutokomeza Mafuta yatokanayo na mabaki ya wanyama. 
Saba, kuanzishwa kwa kanuni ya mwingiliano wa usawa wa mifumo yote ya ikolojia.


Na nane, watalaam wanasisitiza umuhimu waufadhili wa kutosha kwa ajili ya shughuli za utunzaji wa baioanwai. 


“Chini ya dola bilioni 100 zinatengwa kila mwaka kwa ajili ya suala hili, ingawa mami ya mabilioni ya dola nyingine zinahitajika.” Imeeleza ripoti hiyo.