Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Heko Rwanda kwa uzinduzi wa Gen U, ni hatua kubwa:UNICEF 

Kutoka Kusoto Rais wa Bank Kuu, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Rais wa Rwanda Paul Kagame , Mkuu wa UNICEF na balozi mwema wa UNICEF Lily Singh kwenye tukio la ngazi ya juu la uzinduzi wa mkakati wa Umoja wa Mataifa wa vijana Generation Unlimited (Gen U
UN Photo/Mark Garten)
Kutoka Kusoto Rais wa Bank Kuu, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Rais wa Rwanda Paul Kagame , Mkuu wa UNICEF na balozi mwema wa UNICEF Lily Singh kwenye tukio la ngazi ya juu la uzinduzi wa mkakati wa Umoja wa Mataifa wa vijana Generation Unlimited (Gen U

Heko Rwanda kwa uzinduzi wa Gen U, ni hatua kubwa:UNICEF 

Malengo ya Maendeleo Endelevu

Shirika la umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limeipongeza serikali ya Rwanda na watu wake kwa kuzindua mkakati wa kikazi kisicho na ukomo au Generation Unlimited (Gen U).  

Kupitia ujumbe maalum kwa serikali na watu wa Rwanda mkurugenzi mtendaji wa UNICEF Henirietta Fore amesema “Hongera sana Rwanda hii ni hatua kubwa kwa vijana nchini humo.Ubia wa Gen U ni kitu cha kipekee, na inamaanisha kwa mara ya kwanza sekta za umma na binafsi zinaungana kushughulikia changamoto za dunia.” 
 
Bi. Fore ameongeza kuwa vijana wanakosa ujuzi, mafunzo na elimu wanayohitaji ili kufanikiwa katika soko la kimataifa. 
 
Lakini Rwanda kwa mfano hivi sasa msingi wa viwanda unakua lakini vijana sio wakati wote wanapata ujuzi unaohitajika katika soko la ajira ili kuweza kuwa sehemu ya ukuaji huo.  
 
Ameongeza kuwa hivi sasa mambo yanabadilika “kwani chini ya uongozi wa Rais Kagame serikali inachukua hatua kuhusu hilo. Inawekeza katika masuala ya kiufundi, elimu ya kujitegemea na mafunzo. Inawasaidia wahitimu wa vyuo vikuu na nyenzo za kuanzisha biashara zao wenyewe. Hii ni hatua muhimu”.
 
Rais Paul Kagame wa Jamhuri ya Rwanda akihutubia mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani tarehe 24 Septemba 2019
UN Photo/Cia Pak
Rais Paul Kagame wa Jamhuri ya Rwanda akihutubia mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani tarehe 24 Septemba 2019
 Mkuu huyo wa UNICEF amesema na leo hii kujiunga na ubia wa Gen U, ni hatua muafaka kwani kupitia ubia huo serikali na sekta binafsi nchini Rwanda zitafanya kazi pamoja kubaini na kusongesha suluhu bunifu ambazo zinaweza kutoa ujuzi, mafunzo na elimu kwa ufanisi zaidi katika majukwaa mbalimbali mtandaoni ili vijana waweze kuyapata mafunzo hayo hata wakiwa mbali suala ambalo ni muhimu sana hasa wakati huu wa janga la corona au COVID-19.
 
Amesisitiza kwamba Gen U inahimiza katika kuwekeza kwenye nyenzo na programu ambazo zinasaidia kujenga uwezi wa kidijitali wa karne ya 21 ambao unahitajika leo hii katima biashara mbalimbali duniani, pia inahimisa mafunzo kwa viteno, uangenzi na programu za kuwaunganisha vijana wenye ujuzi na ajira muafaka kwani ni ushirika unaozingatia maslahi ya kizazi kichanga. 
 
“Na hii ni kwa sababu uwekezaji wa serikali, sera , seria na mipango yake ina ukomo. Tunahitaji ubunifu, mawazo na mchango wa sekta inafsi kutusaidia, Gen U ni ushindi kwa kila mtu. Kwa makampuni ya viashara yanayohitaji watu waliopata mafunzo mazuri, wenye ujuzi, kwa serikali ambayo inataka kuanzisha fursa za kiuchumi na kuendeleza taifa na la msingi zaidi kwa vijana ambao ni mustakbali wa kila nchi.” 
 
Kwa mantiki hiyo Bi.Fore amesema Rwanda leo hii imechukua hatua muhimu ya kuwasaidia vijana hao kwa kuzindua Gen U na UNICEF inajivunia kushirikiana na Rwanda katika safari hii na kuendelea kuzalisha fursa mpya kwa vijana, kuwapa nyenzo wanazohitaji ili kujenga vyema mustakbali wao.