UNHCR kuendeleza huduma licha wadau wake wa kibinadamu kufungiwa Uganda

8 Septemba 2020

Shirika la Umoja wa Mataifala Kuhudumia wakimbizi, UNHCR nchini Uganda limesema linajitahidi kuhakikisha kwamba hatua ya serilkali ya kuyasimamisha mashirika ya misaada yasiyo ya kiserikali 208 nchini humo kwa kutokidhi vigezo vya sheria kuhudumia wakimbizi , haiathiri utoaji wa huduma kwa wakimbizi hao.

UNHCR imesema inafuatilia kwa karibu hali katika makazi yote ya wakimbizi ili kuhakikisha mwendelezo wa utoaji wa huduma muhimu kati ya changamoto za COVID-19  baada ya  serikali kusitisha huduma za wadau wa UNHCR wanaohudumia  wakimbizi.

Mratibu mwandamizi wa mahusiano ya nje kwenye UNHCR Uganda Laslie Velez, amesema wanayahimiza mashirika yote ambayo bado hayajatimiza vigezo vya kisheria kutimiza vigezo hivyo, tunaendelea kufuatilia kwa karibu ili kuzuia madhara yake kwa huduma za wakimbizi na jamii zinazowahifadhi ambacho ni kipaumbele chetu namba moja. Kwa sasa huduma hizo hazijaathirika. Tuna mashirka wadau wetu 69  yalio shupavu makambini na tumebaini kuwa yanazingatia maagizo yote ya kutekeleza sghughuli za kuhudumia wakimbizi”

Kulingana na Laslie, wanatambua mchango mkubwa wa mashirika yasio ya kiserikali katika kuhudumia wakimbizi.

Wiki iliopita Waziri wa kushughulikia majanga na wakimbizi wa Uganda Hilarry Onek aliagiza mashirika hayo kusitisha huduma zao kwneye makazi yote ya wakimbizi juu ya mikataba yao ya maelewano kupitwa na wakati kinyume na sheria za kuhudumia wakimbizi.

Bi Laslie wa UNHCR amesema shirika hilo linakaribisha hatua hiyo ya serikali kwani nalo lisingependa kushirikiana na mashirika yasiyozingatia sheria za nchi husika, “huduma zote zinaendelea kama ilivyopangwa. Tunakaribisha juhudi za serikali kuhakikisha kwamba mashirika yote ya kutoa huduma za kibinadamu kwa jamii za wakimbizi yana mikataba ya makubaliano na ofisi ya serikali inayohusika na masuala ya wakimbizi,”

Uganda inahifadhi wakimbizi zaidi ya milioni moja nukta mbili kwa sasa, wengi wakiwa walikimbia mizozo katika nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Sudan Kusini na Rwanda.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter