Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi za Afrika zashiriki mkakati mkubwa wa chanjo ya COVID-19 :WHO 

Utafiti wa kutafuta Chanjo ya virusi vya Corona unaendelea
Unsplash
Utafiti wa kutafuta Chanjo ya virusi vya Corona unaendelea

Nchi za Afrika zashiriki mkakati mkubwa wa chanjo ya COVID-19 :WHO 

Afya

Wakati mbio za kusaka chanjo salama na inayofanya kazi dhidi ya janga la corona au COVID-19 zikiendelea kote duniani, nchi za Afrika zinajisajili katika mkakati mkubwa wenye lengo la kupata takriban dozi milioni 220 za chanjo kwa ajili ya bara hilo pindi leseni ya chanjo hiyo itakapotolewa na kuidhinishwa. 

Hayo ni kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO ambalo pia limesema nchi zote 54 za bara hilo zimeonyesha nia ya kujiunga na COVAX ambao ni mkakati wa kimataifa unaoongozwa kwa ushirikiano kwa ajili ya maandalizi ya milipuko ya magonjwa kwa ajili ya ubunifu CEPI, muungano kwa ajili ya chanjo GAVI na WHO

Washirika hao wanafanya kazi kwa karibu na serikali na wazalishaji wa madawa ili kuweza kupata chanjo za kutosha kulinda wale walio hatarini zaidi katika bara hilo la Afrika. 

Kupitia mchakato wa GAVI inayoratibu kitengo cha COVAX, mkakati wa kuhakikisha upatikanaji wa chanjo kwa wote, katika nchi za kipato cha juu na cha wastani ambazo zitafadhili ushiriki wao na zile za kipato cha chini ambazo ushiriki wao utapigwa jeki na ahadi ya soko la COVAX ijulikanayo kama (AMC). 

Nchi zitakazojifadhili Afrika 

Hadi sasa kuna nchi 8 barani Afrika ambazo zimekubali kujilipia dozi za chanjo zao kupitia kituo cha COVAX. 

Ni hii itageuka kuwa mkataba wa kujiunga na mkakati huo ifikapo Septemba 18 na kufuatiwa na malipo ambayo ni lazima yatolewe sio zaidi ya  tarehe 9 Oktoba 2020. 

“Equatoria Guinea imejisajili kwa COVAX kama ndio njia pekee itakayohakikisha watu wetu wanaweza kupata chanjo ya COVID-19. Tunahofu kwani baadhi ya nchi tajiri zimechukua hatua ili kukidhi matakwa yao. Tunaamini kwamba kupitia mradi huu tunaweza kufanikiwa kupata fursa ya chanjo iliyofanyiwa majaribio kwa wakati na kwa gharama ndogo.” Amesema Mitoha Ondo’O Ayekaba naibu waziri wa afya na ustawi wa jamii wa Equatoria Guinea. 

WHO imesema nchi zingine 46 zinakidhi masharti ya kupata msaada kutoka kwa chombo cha ufadhili cha COVAX AMC ambacho kimeshakusanya takriban dola milioni 700 katika lengo la awali la dola bilioni 2 zinazohitajika kwa ajili ya ufadhili kutoka kwa nchi tajiri wahisani , alikini pia sekta binafsi na wafadhili wengine ifikapo mwisho wa mwaka huu wa 2020. 

Kwa ushirikiano mamilioni ya maisha yataokolewa 

Mkurgenzi wa WHO kanda ya Afrika Dkt. Matshidiso Moeti amesema “COVAX ni mkakati wa aina yake wa kimataifa ambao utazijumuisha nchi za afrika na kuhakikisha kwamba hawaachwi nyuma ya foleni kwa ajili ya chanjo ya COVID-19. Kwa kwenda nje ya bara hili ili kushirikiana na serikali na makampunni watengenezaji wa madawa katika kiwango cha kimataifa na kushawishi uwezo wa kununua, nchi zinaweza kuwalinda watu walio hatarini zaidi baranoi Afrika kutokana na ugonjwa huu.” 

CEPI inaongoza utafiti wa chanjo wa COVAX na unalenga kutengeneza chanjo hadi tatu ambazo zitakuwa salama na zinazofanyakazi ambazo zitapelekwa kwa nchi zinazoshiriki kwenye mkakati wa COVAX. 

Kwa sasa kuna uwezekano wa chanjo tisa tisa zinazoungwa mkono na CEPI na mbili ziko katika majaribio ncini Afrika Kusini, na pia kwenye kanda nyingine kote duniani. 

Dkt. Richard Hatchettmtendaji mkuu wa CEPI amesema “Ni muhimu kwa nchi barani Afrika kushiriki katika chanjo za majaribio ikiwa ni oamoja na majaribio mengine yanayofayika katika kanda zingine duniani. Majaribio ya chanjo katika bara hilo yatahakikisha kwamba takwimu zinakusanywa kuhusu usalama na utendaji wa chanjo hiyo ya matarajio kwa ajili ya Afria pindi itakapohakikiwana kuidhinishwa. CEPI inawekeza katika utafiti na utengenezaji wa aina mbalimbali za uwezekano wa chanjokwalengo la kufikisha chanjo salama na inayofanyakazi kwa wale ambao wanahitaji zaidi kupitia COVAX.” 

Usambazaji wa chanjo za majaribio 

Kupitia COVAX chanjo ambazo zitakuwa zimefaulu masharti ya kupitishwa au mahitaji ya awali ya WHO ili kupitishwa zitapelekwa kwa usawa katika nchi zote zinazoshiriki kwa kuzingatia idadi ya watu wake. 

Kipaumbele cha utoaji chanjo katika nchi hizo kwa mujibu wa WHO kitatolewa kwa waudumu wa afya na wale walio hatarini zaidi na kisha chanjo hiyo sasa itaenda kwa kundi lingine la kipaumbele na baadaye kwa umma wote katika nchi zinazoshiriki mkakati huo wa COVAX. 

Nchi za Afrika zitahitaji kuwa na mifumo sahihi na miundombinu inayoainisha sheria na maadili kwa ajili ya uidhinishaji wa haraka wa chanjo ya majaribio. 

Zitahitaki kuwa mkakati wa kiufundi na mfumo wa usambazaji ambao sio tu utaweza kuwafikia walengwa wa awali kwa ajili ya utaratibu wa chanjo na kampeni bali kuwa tayari kutoa chanjo kwa idadi kubwa zaidi ya watu. 

“Ili kuendesha chanjo kikamilifu na kwa ufanisi katika nchi za Afrika ni muhimu jamii zikahusishwa na kuelewa mahitaji kwa ajili ya chanjo.” Amesema Dkt. Richard Mihigo meneja wa programu, chanjo na utengenezaji wa chanjo wa WHO ofisi ya Afrika. 

Ameongeza kuwa ni muhimu kuanza kufanyakazi na jamii ili kuandaa njia kwa ajili ya moja ya kampeni kubwa za chanjo kuwahi kushuhudiwa Afrika.